Posts

Showing posts from January 4, 2015

MIMI SI MENEJA TENA WA ROSE MUHANDO-MSAMA

Image
HATIMAYE Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, ameibuka na kutamka yeye si Meneja wa malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando akisema amekuwa akishirikiana naye katika mazingira ya kawaida kama ilivyo kwa waimbaji wengine. Kwa mujibu wa taarifa ya Msama kwa vyombo vya habari jana, yeye akiwa mlezi wa waimbaji wote wa muziki wa Injili, amekuwa akishirikana nao kwa karibu kutokanana nafasi yake katika huduma hiyo ya uimbaji kwa kipindi cha miaka 15. Msama, mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini kutokana na kuandaa matukio ya muziki huo kama Tamasha la Pasaka, uzinduzi wa albamu na Tamasha la Krismas, alisema ameamua kutoa tamko hilo kutokana na malalamiko ya muda mrefu ambayo amekuwa akipata juu ya Rose. "Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi ikiwemo kutoka kwa viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji, kwamba pengine nimekuwa nikimzua Rose (Muhando) katika mtamasha wanayom

Aunt Ezekiel: Mume wangu Hajui kama nina Mimba

Image
Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’ amefunguka kuwa, licha ya ujauzito wake kuwa mkubwa, mume wake Sunday Demonte hana taarifa yoyote juu ya kitumbo hicho.   Akizungumza na mwandishi wetu, Aunt alisema maneno hayo yanaweza kuwashangaza watu lakini ndiyo ukweli wenyewe.   Alidai kuwa yeye na mume wake huyo hawajaachana na hajapewa talaka kama watu wanavyodai lakini hajui kwamba ni mama mtarajiwa na hata akijua hawezi kumuacha.   “ Kiukweli mume wangu hajui kuwa nina ujauzito na hata akijua wala hawezi kuniacha, ananipenda sana. Sijaachana naye na wala sijapewa talaka, hayo yanayosemwa ni umbeya tu, ” alidai Aunt.

HABARI YA MJINI: WAKATI DIAMOND AKIMTESA NA ZALI, WEMA AJIBU MAPIGO!

Image
Habari ya mjini!  Gumzo katika ulimwengu wa mastaa Bongo ni kitendo cha mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuendelea kujiachia na staa wa mrembo mwenye maskani yake nchini Uganda na Afrika Kusini ‘Sauz’, msanii Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’  huku  aliyekuwa ‘kiburudisho’ wa jamaa huyo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akijibu mapigo kwa kumnasa mwigizaji Joseph Van Vicker wa Ghana, Ijumaa lina sarakasi nzima.  Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye akimbusu Van Vicker kimahaba.   WEMA ATIMKIA GHANA Wakati Diamond akitimkia Marekani kwenda kutumbuiza kwenye sherehe za 53 za Uhuru wa Tanganyika kwa Wabongo waishio nchini humo (Diaspora), Desemba 9, mwaka  huu , Wema yeye alitimkia kwenye Mji Mkuu wa Ghana jijini Accra kuungana na Van Vicker kwa ajili ya ‘projekti’ kama ilivyokuwa kwa Diamond na Zari.  Habari za uhakika zilizothibitishwa na Wema mwenyewe zilieleza kwamba yupo nchini humo kwa ajili ya kurekodi fila

PENNY: NATAMANI MTOTO, SINA WA KUZAA NAYE

Image
Stori: Imelda Mtema Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye. Penniel Mwingilwa. Penny alitoa tamko hilo baada ya Diamond kunukuliwa jana (Alhamisi) na gazeti dada la hili, Amani kuwa, alimpa mimba mara mbili binti huyo lakini zikayeyuka katika mazingira ya kutatanisha. Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Penny alisema, sasa hivi anapomuona mtoto anachanganyikiwa na kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi. “ Kiukweli sasa ndiyo ule wakati wa kuzaa, natamani sana mtoto lakini sasa wa kuzaa naye yuko wapi? Hapo ndiyo tatizo maana siyo kuzaa na mtu ili mradi mtoto awe na baba,” alisema Penny .

HIVI NDIVYO MADAHA ALIVYOFUNGUKA KUHUSU SKENDO YA KUJIUZA, KUTOKUWA NA PA’ KUISHI

Image
Baby Joseph Madaha ndiye ambaye wiki hii yuko hapa kujibu maswali 10 ambayo mwandishi wetu Gladness Mallya alimuuliza. Ilikuwa hivi; Staa Baby Joseph Madaha. Ijumaa: Umekuwa ukitajwa kuwa wewe ni msanii wa kike unayeongoza kwa kubadilisha mabwana kila kukicha, hili likoje? Baby Madaha: Ukweli hiyo huwa inatokea tu na huwa sipendi kusumbuliwa na mwanaume, nikiona ananizingua nammwaga. Hata hivyo, kwa sasa nimeamua kutulia kwanza, nafanya kazi, mapenzi pembeni. Ijumaa: Unadhani kwa nini umekuwa ukiingia kwenye uhusiano kisha kutoswa, ni umachepele wako au kitu gani? Baby Madaha: Mimi wala siyo machepele kama watu wanavyonifikiria na kiukweli huwa nawaacha mimi na siyo wao kuniacha. Ijumaa: Mpaka sasa umeshakuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wangapi? Baby Madaha: Wanaume niliotembea nao ni siri yangu kwa sababu nikitaja idadi hapa watu watalia na wewe mwandishi unaweza kuzimia. Ijumaa: Kuna tetesi kwamba wewe na msanii mwenzako Isabela Mpanda huwa mnaishi kama

Mwana wa Raila Odinga afariki

Image
Fidel Castro Fidel Odinga mwana wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amepatikana akiwa amefariki nyumbani kwake huko Karen. Maafisa wa polisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mfanyibiashara huyo ambaye pia amekuwa akionekana katika ulingo wa kisiasa. Maafisa wa Polisi wanasema kuwa uchunguzi wa mapema umeonyesha kuwa Fidel alikuwa nje usiku wa jumamosi na alirudi mapema jumapili. Aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga. Haijulikani ni nini kilichosababisha kifo chake. Kundi la wabunge pamoja na maseneta liliwasili katika nyumba ya Raila baada ya kupata habari hizo. Maafisa wanaosimamia kesi hiyo wanasema kuwa wanataka kujua ni wapi Fidel alikuwa usiku wa jumamosi na alikuwa na nani.

DIAMOND ATEULIWA KUTUMBUIZA TUZO ZA MWANASOKA BORA CAF

Image
Msani Nasib Abdul ‘Diamond’ amechaguliwa kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye hafla ya utoaji tuzo za mwanasoka bora Afrika 2014. Diamond atatumbuiza katika tuzo hizo ambazo wachezaji 25 nyota barani Afrika wamechaguliwa kugombea tuzo hizo. Hafla hiyo itafanyika Januari 8, 2015 jijini Lagosi Nigeria.  Mwanasoka Bora, Yaya Toure raia wa Ivory anayeitumikia Manchester City ya England ni kati ya watakaowania nafasi hiyo.  Wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika: 1.      Ahmed Musa                              (Nigeria, CSKA Moscow) 2.      Asamoah Gyan                           (Ghana, Al Ain) 3.      Dame N’doye                             (Senegal, Lokomotiv Moscow) 4.      Emmanuel Adebayor                  (Togo, Tottenham) 5.      Eric Maxim Choupo-Moting             (Cameroon, Schalke 04) 6.      Fakhreddine Ben Youssef               (Tunisia, CS Sfaxien) 7.      Ferdjani Sassi                             (Tunisia, CS Sfaxien) 8.      Y