Posts

Showing posts from November 13, 2017

Sababu za Mbowe kutomuheshimu Lipumba hizi hapa

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amedai kwamba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ni Profesa wa ajabu ambaye anaweza kubomoa chama alichokijenga. Akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Mtwara, Mh. Mbowe amesema kwamba hana ugomvi wowote na Prof Lipumba ingawa amekiri atakuwa muongo akisema kwamba anamuheshimu kwani anatumika katika kukivuruga chama alichokuwa akikiongoza kwa muda mrefu. Mh. Mbowe amesema kwamba wakati CUF ikishirikiana na UKAWA kwa ujumla kutafuta kura na kuongeza wabunge wa chama hicho bungeni, yeye Prof Lipumba alikuwa mafichoni na anamshanga sasa hivi anavyorudi ndani ya chama hicho na kutaka kukisambaratisha. "Sina ugomvi na Prof Lipumba lakini nikisema namuheshimu nitakuwa muongo sana. Prof Lipumba ni msomi sana tena msimchezee kwenye elimu lakini usomi ni jinsi unavyotumia elimu yako lakini siyo wingi wa vyeti. Ni Profesa wa aja

Baada ya hukumu Lulu, Mama Kanumba afunguka

Image
Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na kusema kwamba leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipoziikwa mwanaye ili kwenda kumzika upya. Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo. "Kwa sasa sina la kusema ila  naishukuru sana Mahakama kwa kutenda haki, pia niishukuru sana Serikali yangu lakini pia nikitoka hapa nitakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika upya mwanangu Kanumba". Mama Kanumba. Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake. Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.

Zitto aizungumzia Bombadier Bungeni

Image
Serikali imekiri kujitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji wa shughuli za serikali kwa uwazi (OGP), ambao serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijiunga Septemba 21 mwaka 2011. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mh. George Mkuchika wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe lililohoji kwanini serikali imejitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji serikali kwa uwazi (OGP). Mh. Mkuchika amesema baada ya serikali kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa, ambapo ameongeza kuwa sio nchi ya kwanza kujitoa kwenye mpango huo. “Baada ya serikali kushiriki utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa, na Tanzania sio nchi pekee iliyojitoa, zipo nchi kama Hungury na Urusi zilijiunga na baadae kujitoa”, amesema Waziri Mkuchika. Kwa upande mwingine Mh. Zitto ameshauri kuwa serikali ingeendelea kuwa mwanachama wa (OGP) ingefaidi

Breaking News: Lulu ahukumiwa kwenda jela

Image
Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemhukumu kwenda jela miaka miwili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia. Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa anaendesha kesi hiyo, na kusema kwamba mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira, hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela. "Ushahidi wa mazingira unaweza kutumika kama msingi pekee wa kumtia hatiani mshtakiwa tena mshtakiwa pekee, sasa ninapokwenda kuangalia maelezo ya mshtakiwa kama yanakidhi vigezo nilivyosema awali, kwa mujibu wa mshtakiwa alisema alianza kupigwa na marehemu, marehemu alilewa lakini mshtakiwa alitakiwa kutoa maelezo yanayo jitosheleza, kwa hili mshtakiwa alijikanganya", amesema Jaji Rumanyika. Jaji Rumanyika ameendelea kwa kusema kwamba.."mshtakiwa katika maelezo yake hakueleza kuwa marehemu alianguka au laah wakati anamkimbiza, mae

Orodha kamili ya washindi wa tuzo za AFRIMA 2017

Image
Zoezi la ugawaji wa tuzo za muziki za AFRIMA (All Africa Music Awards) kwa mwaka 2017 limehitimishwa jana nchini Nigeria katika Hoteli ya Eko.Mastaa kadhaa wameweza kujishindia tuzo hiyo kubwa ya muziki kama vile Wizkid, Simi, M.I, Tiwa Savage, Ycee, Orezi, 2Baba, Alikiba na wengineo. Kwa upande wa Wizkid aliondoka tatu ambazo ni Song of the Year, Artist of the Year & Best West African Act (Male), na kwa msanii Alikiba aliondoka na tuzo mbili Best Africa Collaboration na Best Artist or Group in Africa RnB and Soul. Orodha kamili ya washindi; Best Central African Act (Male) – Locko Best Central African Act (Female) – Montess Best East African Act (Male) – Eddy Kenzo Best East African Act (Female) – Nandy Best Southern Africa Act (Male) – Emtee Best West African Act (Male) – Wizkid Best West African Act (Female) – Tiwa Savage Best African Collaboration – Alikiba feat M.I – “AJE“ Best Artist in African Rock – Gilad Millo (Kenya) Best Artist or Grou