TRA yaanika deni la Acacia, ni sawa na 'bajeti ya miaka 13'
Mamlaka ya Mapato (TRA) imeitaka Kampuni ya Acacia kulipa zaidi ya Sh424 trilioni kutokana na ukwepaji kodi ilioufanya kuanzia mwaka 2000. Kwa kutumia bajeti ya sasa, fedha hizo ni sawa na bajeti ya Tanzania ya miaka 13. Deni hilo, ambalo ni sawa na dola 190 bilioni za Kimarekani limetokana na hesabu zilizopigwa kwa kutumia taarifa iliyotolewa na kamati mbili zilizoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza usafirishaji wa mchanga wa madini unaofanywa na kampuni hiyo kutoka migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi. Taarifa iliyotolewa jana na kampuni hiyo imekataa kulipa deni hilo kwa maelezo kwamba haijapewa ripoti ya kamati zote mbili. “Hatuyakubali makadirio haya. Kampuni itaangaalia haki na namna zote zilizopo kuhusu suala hili,” inasema taarifa hiyo. Kwa mujibu wa Acacia, deni hilo limeelekezwa kwa kampuni zake tanzu ambazo ni Bulyanhulu Gold Mine (BGML) inayoendesha mgodi wa Bulyanhulu, na Pangea Minerals (PML) inayosimamia mgodi wa Buzwagi. Taarifa hiyo iliyo...