HIZI NDIO KAULI ZA MBATIA AKIHTUBIA KUPITIA RUNINGA USIKU HUU
- Mbatia analalamikia vitisho vya Mgombea wa CCM, Magufuli kuwa wakiwachagua wapinzani nchi itaingia kwenye machafuko - Mbatia: Watu wameanza kupoteza maisha, wana UKAWA wanadhalilishwa na wengine kutekwa - Mbatia: Hali imeanza kuwa tete, vitisho vya kila aina vimeanza. Tumedhalilishwa sana, tumeitwa matusi ya kila aina. - Mbatia: Lowassa si mdini, alikuwa anataka watanzania wamwombee. Mhe. Lowassa hajaenda kwenye nguvu za giza. Hajatumia viungo vya albino, ameenda kuomba viongozi wa dini wamwombee; udini wake unatoka wapi? - Mbatia: Tunawashukuru Lowassa na Sumaye kwa nia zao njema kuja Upinzani kuongeza nguvu ili tuyafanye mabadiliko ya kweli - Mbatia: Hata CCM wangemweka malaika, si rahisi kupata mabadiliko bila kufanya mabadiliko ya mfumo. - Mbatia: CCM wanasema usichague chama, chagua mtu. Watanzania wanatakiwa kujua kuwa Magufuli ni CCM, na hawezi kujitenganisha na CCM. Huwezi kulisukuma gari ukiwa ndani yake, lazima utoke ndipo ulisukume. Mabadiliko ndani ya CCM hayaw...