Posts

Showing posts from May 7, 2015

RECHO WA THT ALIA NA BABU TALE BAADA YA KUZUIWA KUMTUNZA DIAMOND.

Image
MREMBO mwenye sauti nyororo kutoka Jumba la Kukuza Vipaji Tanzania (THT), Winifrida Josephat ‘Recho Mapenzi,’ hivi karibuni alijikuta akiangua kilio baada ya kuzuiwa kupanda kwenye jukwaa kwa ajili ya kumtunza Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz.’ Mrembo mwenye sauti nyororo kutoka Jumba la Kukuza Vipaji Tanzania (THT), Winifrida Josephat ‘Recho Mapenzi. Tukio hilo lilitokea ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar kwenye shoo ya Zari All White Party ambapo bidada huyo akiwa katika hali ya mzuka alijikuta akiishia kuangua kilio baada ya kuzuiwa na Meneja wa Diamond, Babu Tale kupanda jukwaani. Akilalama kwa machungu baada ya kukwamishwa kumfikia Diamond, Recho alisema kuwa hakufurahishwa hata kidogo na uamuzi wa Babu Tale kwani anamjua wazi ni msanii hivyo hakuwa na haja ya kuwaamuru mabaunsa kumzuia kwenda kumtuza staa mwenzake. “Kweli Tale hajanitendea haki hata kidogo, kwani nilimuahidi mapema Diamond ningemtuza na pale nilitaka kutimiza ahadi ...

YULE BI HARUSI ALIYETOROKA SIKU MOJA BAADA YA KUFUNGA NDOA ANASWA LIVE.

Image
YULE mwanamke Tatu Ally, mkazi wa Kongowe, Mbagala jijini Dar aliyefunga ndoa na kutoroka kwa mumewe aliyetajwa kwa jina moja la Ramadhan, mkazi wa Mbezi-Kimara, amenaswa baada ya msako mkali uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na ndugu zake. Stori ya Tatu kutoroka kwa mumewe siku moja baada ya kufunga ndoa iliripotiwa na gazeti hili wiki iliyopita, ukurasa wa nyuma, ikiwa na kichwa cha habari kilichosomeka:BI HARUSI AFUNGA NDOA, ATOROKA. Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika kilieleza kuwa, Tatu alikutwa na mwanaume mwingine maeneo ya Toangoma, Kigamboni, Dar na kujitetea kuwa aliamua kutorokea kwa mwanaume huyo kwa kuwa ndiye mchumba’ke wa siku nyingi na alikuwa amesafiri kwa muda tu. “Kweli Tatu amepatikana na alipelekwa moja kwa moja kwenye Kituo cha Polisi cha Kongowe-Mwisho, huku akiwa na huyo anayedai ni mchumba’ke wa siku nyingi (jina halikupatikana).Ilisemekana kwamba, Tatu akiwa mikononi mwa polisi alinena kuwa mwanaume huyo alikuwa amesafiri kwa muda na ...

MADEREVA WAPEWA KIPAUMBELE KWENYE KAMATI YA KUSIMAMIA USAFIRISHAJI.

Image
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano wa wandhi wa habari na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.) Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii. Madereva wamepewa kipaumbele kwenye tume itakayokuwaikisimamia usafirishaji,kwani tume hiyo itakuwa na wajumbe watano kutoka Umoja wa madereva tuu na kutoka sekta nyingine watakuwa wajumbe watatu . Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Makonda amesema kuwa kamati hiyo haitaundwa na serikali, wajumbe watatokana na uchaguzi wa madereva wenyewe pia na wajumbe wengine watatoka Mamlaka ya usafirishaji (SUMATRA), TABOA , TATOA, Wizara ya Ajira, wizara ya na mambo ya ndani. Makonda ameongezea kuwa Mg...

MREMBO ABABULIWA ‘RECEPTION’ NA MTALAKA WA BOSI WAKE JIJINI DAR

Image
INASIKITISHA sana! Muuza baa mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Halima, anajiuguza vidonda vikubwa mwilini vilivyotokana na kumwagiwa maji ya moto na mwanamke ambaye ni mtalaka wa bosi wake ambaye ndiye mmiliki wa baa anayofanyia kazi, Amani linakupa zaidi. Halima anayedaiwa kumwagiwa maji ya moto. Kwa mujibu wa chanzo ambacho ni ndugu wa majeruhi huyo, tukio hilo lilijiri mwezi uliopita ndani ya baa moja maarufu iliyopo maeneo ya Ubungo, Dar es Salaam ambapo majeruhi huyo anafanyia kazi baada ya mwanamke huyo kuamini Halima anatembea na mtalaka wake. Inadaiwa kuwa, mwanamke huyo ambaye ni mtuhumiwa na mwanaume mmiliki wa baa aliyejulikana kwa jina moja la Mushi waliachana miaka mingi iliyopita.“Lakini mwanamke akawa anamfuatilia mumewe kila siku na kwa kila kitu. Ilifika mahali akaambiwa kuwa, mwanaume huyo aliyetengana naye ana uhusiano wa kamapenzi na baamedi wake mmoja.” “Ndipo siku ya tukio, mwanamke huyo alifika kwenye baa hiyo akitoka kusikojulikana. Wakati h...

ANGALIA MVUA ZINAVYOKWAMISHA SHUGHULI ZA WATU JIJINI DAR

Image
Wananchi wakijaribu kuvuka barabara eneo la Sinza, Afrika sana leo asubuhi. Mwanafunzi akionekana akipita katika barabara iliyojaa maji eneo la Afrika Sana. Baadhi ya wananchi wakionekana kutafakari namna ya kupita eneo la Sinza Afrika Sana. Kijana aliyeko upande wa kushoto ambaye hakufahamika jina lake haraka, akivusha wananchi kwa kiasi cha shilingi mia mbili (200) eneo la Afrika Sana. Magari pamoja na Bajaji zikionekana kupita kwa tabu katika barabara iliyojaa maji. Vijana wakiendelea kuvusha raia kwa kiasi cha shilingi mia mbili (200) eneo la Afrika Sana.MVUA zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, zimeleta mafuriko katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo na kusababisha adha kwa wakazi wake huku barabara zikiwa zinapitika kwa tabu na zingine kutopitika kabisa.

LULU AFUNGUKA NA KUDAI ''MIMI SINA JINI MAUTI JAMANI''

Image
MSANII nyota wa filamu, Elizabeth Michael `Lulu’ amekanusha uvumi kuwa matatizo yanayowatokea wanaume aliowahi kuwa nao yanatokana na yeye kuwa na Jini Mauti anayesababisha hali hiyo kutokea, Amani linakujuza.   Msanii nyota wa filamu, Elizabeth Michael `Lulu’.Akizungumza na gazeti hili juu ya madai ya wadau mbalimbali kuhusiana na matukio mengi yanayomtokea, muigizaji huyo wa filamu ya Foolish Age, alisema maisha yake ya siku hizi ni ya kusali sana, hivyo anaamini kutokana na maombi yake, hali yake iko vizuri kutokana na Mungu kumpa anachokihitaji. “Ninasali sana kwa sasa aisee, mara nyingi nafanya hivyo mara tatu kwa siku, ninao uwezo wa kukemea mapepo na yakaondoka, hayawezi kukaa mwilini mwangu,” alisema muigizaji huyo ambaye miaka michache iliyopita, aliondokewa na mpenzi wake, Steven Kanumba aliyeanguka na kufariki mbele yake. Mtabiri mmoja maarufu jijini Dar es Salaam, Maalim Hassan Yahya Hussein, alisema tatizo kubwa linalomsumbua binti huyo ni jini maut...

ADEBAYOR AVIANIKA VISA VYA FAMILIA YAKE NA INAVYOMCHUMA FEDHA, BARUA YAKE YASIKITISHA WENGI, IMETAFSIRIWA KISWAHILI HAPA

Image
Mshambuliaji wa Tottenham, Emmanuel Adebayor ameandika maelezo marefu kwenye akaunti yake ya Facebook kuelezea visa anavyofanyiwa na familia yake wakiwemo mama, kaka na dada zake. Adebayor anawashutumu ndugu zake kwa tamaa ya mali zake. Licha ya kuwafanyia mambo mengi ikiwemo kuwajenga nyumba, kuwanunulia magari na kuwapa mitaji ya biashara, wameendelea kumtupia shutuma nyingi. Tumeitafsiri post hiyo kwaajili yako. Sehemu ya maelezo hayo marefu inasema: SEA, nimezihifadhi habari hizi kwa muda mrefu lakini nadhani leo ni muhimu kuziweka wazi baadhi yake kwenu. Ni kweli masuala ya kifamilia yanapaswa kusuluhishwa ndani kwa ndani na sio hadharani lakini nafanya hivi ili pengine familia zote zinaweza kujifunza kutokana na kile kilichotokea kwangu. Pia weka akilini kuwa hakuna chochote kati ya haya kinahusiana na pesa. Nikiwa na miaka 17, kwa mishahara yangu kama mcheza soka, nilijenga nyumba kwaajili ya familia yangu na kuhakikisha kuwa wapo salama. Kama nyote mn...