Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal afungua mkutano wa Mabunge ya SADC mjini Arusha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia vikundi vya sanaa vya ngoma za aina mbalimbali alipowasili katika Jengo la Ukumbi wa mikutano A I C C mjini Arusha kwa ajili ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC leo Octoba 20, 2013. (Picha na OMR) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbles Lema nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C Arusha, Baada ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC katika ukumbi wa A I C C mjini Arusha leo 20 Octoba 2013. Kushoto Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa wawi kisiwani Pemba Mhe Hamad Rashid nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C Arusha, Baada ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanac...