Posts

Showing posts from August 30, 2013

ANGALIA PICHA ZAIDI YA 30..KATIKA UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA DIAMOND

Image
Hamis Mwinjuna A.k.a Mwana F.A alikuwepo pia kushow Love.... Interiew zinahusika sana sehemu kama hizi.... Sauda wa Bongo Beats ya Star Tv nae akukosekana ndani ya nyumba..... Chege Chigunda Toka TMK nae alikuwepo..... Flowers awakosekanagi sehemu kama hizi....... wakiongozwa na Number One Diva Hamisa hassani Mobeto. Mzee Muhidini Gurumo nae akukosekana ndani ya Nyumba.....Furaha Ilioje kumuona Nguli wa Muziki wa Dansi nchini akiudhuria kwenye kitu chako,binafsi nimefurahi sana uwepo wake ulizidi kuimarisha moyo wangu. Prince Brother Man Dully Sykes akiwasili ndani ya Nyumba pembeni na FloweR Shadee toka Clouds Tv,presenter wa Cloud 9... Shadee & Dully...Mmmmmh....??? Aya sina usemi Kama kawaida...... Sarah A.k.a Shaa nae ndani  Movement zikiendelea na mahojiano mbalimbali kati ya wasanii na presenters wa vituo mbalimbali vya Habari & Blogs kiujuml...

ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA

Image
Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita. Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika  kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam. Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu. Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi. BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.  MJUE ASKOFU MOSES KULOLA Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma sh...

SHEIK PONDA AFIKISHWA MAHAKAMANI TENA.....KESI YAAAHIRISHWA HADI SEPTEMBA 11

Image
Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda jana alisababisha kusimama kwa shughuli za Serikali wilayani Morogoro baada ya ofisi kadhaa ikiwamo ya Mkuu wa Wilaya na baadhi ya mitaa kufungwa ili kupisha kusikilizwa kwa kesi inayomkabili katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro.    Tofauti na Agosti 19, mwaka huu wakati aliposafirishwa kwa helikopta, jana Sheikh Ponda alisafirishwa kwa barabara kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro akiwa chini ya ulinzi. Mbali ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro kufungwa, nyingine ni Hazina Ndogo, Madini, Posta, Vipimo, Ukaguzi na Maktaba ya Mkoa.   Sababu za kufungwa kwa ofisi hizo pamoja na Mtaa wa Stesheni na maeneo ya Posta ni kuwa jirani na Mahakama hiyo. Magari yalizuiwa kutembea katika njia na maeneo ya karibu na ofisi pamoja na Mahakama hiyo huku kukiwa na idadi kubwa ya askari polisi na magereza kwa muda wote wa takriba...

AMREF YAANDAA CHAKULA CHA HISANI KUCHANGISHA FEDHA ZA KAMPENI YA “STAND UP FOR AFRICAN MOTHERS”

Image
Mkurugenzi wa Taasisi ya AMREF Tanzania Dk.Festus Ilako akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu  halfa ya chakula cha hisani ya kuchangisha fedha itakayokuwa na kauli mbiu ya “Stand for African(Tanzania) Mother’s ili kuchangia mfuko wa kuwasaidia wakina mama na watoto,halfa hiyo itafanyika Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Bi.Teddy Mapunda  na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa AMREF Tanzania Dk, Rita Noronha. Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Bi.Teddy Mapunda  akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu halfa ya chakula cha hisani ya kuchangisha fedha itakayokuwa na kauli mbiu ya “Stand for African(Tanzania) Mother’s ili kuchangia mfuko wa kuwasaidia wakina mama na watoto,halfa hiyo imeandaliwa na AMREF wakishirikiana na Montage itafanyika Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Serena Dar es Sa...