MILLEN HAPPINESS MAGESE: ASIMULIA AMBAVYO HAWEZI KUBEBA UJAUZITO, ASEMA YUPO TAYARI KUASILI
Millen Happiness Magese. (ANAJIANDAA, anaonekana kuwa ni mtu mwenye hisia sana kabla ya kuanza kuzungumza, anamuuliza jambo Lucy Ngongoseke maarufu kwa jina la Lucy Kiwele ambaye anamwambia ajikaze azungumze, baada ya sekunde kadhaa anaanza kujielezea…) Naitwa Millen Happiness Magese ni mrembo wa Tanzania na Miss Tanzania wa mwaka 2001, kwa sasa nafanya kazi za mitindo nchini Marekani, kabla sijafika huko nilifanya kazi hiyo Afrika Kusini kwa miaka takribani nane. Nipo chini ya Kampuni ya Ford Models, nilisaini mkataba wa miaka minne na baada ya hapo nikasaini tena miaka miwili na ndiyo nilipo mpaka sasa. Miss Tanzania Mwaka 2001, Happiness Millen Magese akiwa ndani ya Global. Millen Magese Foundation Hii ni taasisi ambayo lengo kubwa ni kutoa msisitizo katika elimu. Suala hili linanihusu binafsi na ndiyo maana nalifanya kwa moyo, hapa Tanzania nimeanza na Mtwara baada ya hapo nitaendelea mikoa mingine. Hata nilipokuwa Miss Tanzania nililifanyia kazi suala ...