Posts

Showing posts from January 15, 2018

KUFURU! Vee Money na Jux Wamwaga Minoti Harusi ya Shilole

Image
Uchebe na Shilole waati wa harusi yao usiku wa kuamkia leo. COUPLE ya wakali wa Bongo Fleva, Juma Jux na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ usiku wa kuamkia leo wamefanya kufuru baada ya kugawa minoti kwenye harusi, Shilole na Uchebe iliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam. Katika harusi hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao wakiwemo wa Bongo Fleva na Bongo Movies, Couple ya Jux na Vanessa walipata fursa ya kutoa nasaha na kumpongeza Shilole kwa kufunga ndoa pia wakimpongeza Uchebe kwa kumpata mke aliye bora. Jux na Vanessa. Kwa upande wa Jux alisema zawadi kubwa anayoitoa kwa Shilole ni kumsomesha mtoto wake mmoja kwa mwaka mmoja huku Vee Money akisema atamlipia muimbaji huyo kulala katika Hotel ya Nyota Tano ya Kilimanjaro. Baada ya hapo, Jux alichana pochi na kumkabidhi Vanessa mkwanja ambapo aliwavagaa maharusi na kuanza kuwarushia pesa hizo kama zawadi.

Nufaika Na Kilimo Bora Cha Matango

Image
Habari rafiki na karibu sana katika safu hii ya makala za kilimo. Katika somo liliopita tuliangalia juu ya umuhimu wa kutumia mbegu bora na faida zake. Sasa leo tutaangalia kilimo cha matango kwa kutumia mbegu bora inayoitwa Hybrid Cucumber YETU F1 ambayo utaanza kuvuna baada ya siku 45-50 kutoka kupandwa kwake. YETU F1 ni mbegu chotara ambayo ina umbo zuri na hupendwa sana na walaji. Kiasi cha mbegu 300g(Gramu 300) huweza kutosha ekari moja ambayo utainununua kwa shilingi laki tatu(300,000/=) za kitanzania.  UANDAAJI WA SHAMBA. Chagua sehemu iliyo nzuri,na ukipata sehumu ya tifutifu iliyo changanyikana na mchanga itakuwa vizuri zaidi. Pia ukipata sehemu yenye udongo mzito lakini usiwe una tuamisha maji. Lima shamba na hakikisha umelisawazisha vizuri(yaani hallowing),baada yapo panga matuta yako. KIASI CHA MBEGU . Gramu 300 zenye kiasi ya YETU F1 kinatosha kupanda eneo la ekari moja(100m×40m). Na hii aina ya mbegu 1g ina mbegu 30-40. Kabla ya kupanda hakikish