Posts

Showing posts from April 23, 2015

KAMANDA MKUU WA BOKO HARAMU{ ABOU MOJAHID} AUAWA KIKATILI,

Image
Askari wa jeshi la Nigeria Msemaji wa jeshi la Nigeria Meja Jenerali Chris Olukolade amesema kuwa, vikosi vya nchi hiyo vimemuua kamanda wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Boko Haram Abu Mojahid ambaye ameuawa katika mapigano kati ya jeshi la Nigeria na wapiganaji wa kundi hilo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Olukolade ameongeza kuwa, wapiganaji kadhaa wa Boko Haram nao wameuawa katika mapigano hayo. Wakati huo taarifa kutoka Nigeria zinasema kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuukomboa msitu wa Sambisa ambao ulikuwa ngome ya mwisho ya kundi la kigaidi la Boko Haram. Msitu wa Sambisa huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Hayo yanajiri ikiwa Operesheni ya pamoja ya vikosi vya Nigeria, Chad, Cameroon na Niger dhidi ya Boko Haram ikizidi kuendelea huku kukiwa na taarifa kwamba, imekuwa na mafanikio.

HABARI NJEMA KWA WANABLOG, FORUMS WATANZANIANIA JUU UANDIKISHAJI WANACHAMA TBN

Image
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' - TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi. Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka kujiunga fomu hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi. Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,0

WAKUU WA SHIRIKA LA KUPAMBANA NA UFISADI NCHINI KENYA WASIMAMISHWA KAZI

Image
Rais wa serikali ya Kenya, Uhuru Kenyatta. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amewasimamisha kazi wakuu wawili wa shirika linalopambana na ufisadi nchini humo, siku moja tu baada ya bunge kupitisha mswaada inaowalaumu kwa uzembe na utepetevu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Ikulu ya Rais Manoah Esipisu, tume ya maadili na kupambana na ufisadi, itaendelea na kazi yake licha ya kusimamishwa kwa wakuu hao wawili. Wakuu hao ambao ni Mwenyekiti, Mumo Matemu na naibu wake Bi. Irene Keino wamesimamishwa huku uchungunzi ukianzishwa dhidi yao kuhusiana na tuhuma za uzembe wa kazi na kutumia vibaya madaraka yao ikiwemo kujihusisha na ufisadi. Tangazo hilo limetolewa mwezi mmoja baada ya ripoti kutoka ya tume hiyo kuwasilishwa kwa Rais Kenyatta, ripoti iliyosababisha kusimamishwa kazi kwa Mawaziri wanne wa serikali ya Uhuru Kenyatta na Maafisa wengine 12 na Wakuu serikalini ili kupisha uchunguzi ufanyike dhidi yao

KIJANA AMCHINJA MAMA YAKE MZAZI NA KUTOA TAARIFA UONGOZI WA KIJIJI!!-SINGIDA,SHUHUDIA HAPA

Image
Jeshi la Polisi mkoani Singida, linamshikilia Jumanne Yusuph (33), Mkazi wa Kijiji cha Mtamaa ‘A’ Manispaa ya Singida kwa kumuua mama yake mzazi, Tausi Abdalah (56) kwa kumchinja na kisu shingoni, juzi alfajiri katika kijiji hicho. Baada ya kumchinja mama yake, kijana huyu alikwenda kwa mama yake mkubwa kutoa tarifa, kisha tena akaenda kwa mwenyekiti wa kijiji kumjulisha kuwa amefanya mauaji ya mama yake. Kabla ya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo aliwaua ng’ombe watatu wa mama yake kwa kuwacharanga na mapanga. Pia inadaiwa kuwa aprili 16 mwaka huu, mtuhumiwa huyo alifika kwa mama yake na kubomoa sehemu ya nyumba yake kisha akatokomea kusikojulikana.Kabwe Zuberi Zitto (born 24 September 1976), popularly known as Zitto Kabwe, is a Tanzanian politician.He was a member of the opposition party, Chadema, from 1992 until his expulsion in March 2015. He served as a Member of Parliament for the Kigoma North constituency from 2005 to 2015.On 20 March 2015, he officially joined the Al