Posts

Showing posts from January 16, 2018

BREAKING NEWS: POLISI DAR YAKAMATA SILAHA NZITO

Image
JESHI la Polisi kanda Maalumya Dar es Salaam limekamata silaha mbalimbali zikiwemo bunduki, bastola na vifaa vingine vya kufanyia matukio ya uhalifu pamoja na watuhumiwa mbalimbali wa makosa ya uhalifu ambao walikuwa wakijiandaa kutekeleleza matukio hayo. Akizungumza na wanahabari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasaamesema jeshi hilo limekamata silaha aina ya AK 47 na watuhumiwa wawili nyumbani kwa mzee Said Omary (62) baada ya kupata taarifa kuwa kuna wahalifu wanataka kufanya tukio la wizi wa kutumia silaha. Aidha Polisi imewakamata watuhumiwa 2 wa wizi wa magari ambao baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na radio call, kadi 10 za benki mbalimbali, leseni za udereva, master keys 15 ambapo baada ya kuhojiwa walikiri kutekeleza matukio mbalimbali ua uhalifu huku wakionesha magari mawili na pikipiki moja vinavyodhaniwa kuwa ni vya wizi.

Zitto kabwe azuiwa kufanya mkutano wa hadhara

Image
Jeshi la Polisi Kigoma limemzuia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kufanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Uwanja wa Mwanga Community Center, mkoani Kigoma ambao ulipaswa kufanyika leo Januari 16, 2018. Taarifa iliyotolewa na OCD inasema kuwa kiongozi huyo hakufuata utaratibu wa kutoa taarifa ndani ya masaa 48 kabla ya kufanyika kwa mkutano huo jambo ambalo Mbunge Zitto Kabwe amelilamikia na kusema kuwa amezuiwa kufanya Mkutano kinyume na sheria ya Bunge ya mwaka 1988. "Mimi sitaki kuwapa polisi sifa ya kupambana nasi. Tumeahirisha mkutano mpaka siku ya jumamosi Lakini tumewaandikia barua rasmi kuwa sheria waliyonukuu sio sheria halali na haihusiani na mikutano ya Mbunge kwenye jimbo lake la Uchaguzi. Sheria wanayopaswa kunukuu ni sheria namba 3 ya mwaka 1988 kifungu cha 4(1)". Alisema Zitto Kabwe Kufuatia jambo hilo Zitto Kabwe amedai kuwa atamwandikia barua rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai kuhusu suala hil

Breaking: Mbunge Sugu Anyimwa Dhamana, Apelekwa Mahabusu Gerezani

Image
Mbunge Joseph Mbilinyi “Sugu”. MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amepelekwa mahabusu katika Gereza la Ruanda mkoani Mbeya baada ya kukosa dhamana katika kesi ya uchochezi inayomkabili. Sugu na Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya leo Januari 16 na kupelekwa mahabusu leo Jumanne Januari 16, baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Pande kuiomba mahakama kuzuia dhamana kutokana na usalama wa washtakiwa kutokana na kosa walililotenda. Sugu naMasonga wakipelekwa mahabusu. “Kosa walilolitenda washtakiwa ni kutoa maneno ya fedheha yanayomtaja rais kuwa muuaji hivyo wakiwa nje wanaweza kupata matatizo kwa wananchi ambao hawajapendezwa na maneno hayo,” alidai Wakili Pande. Masonga akihutubia. Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alikubaliana na ombi hilo ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa dhamana. Washtakiwa hao wanadaiwa k