Manji Ajitoa Yanga Rasmi
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji. Mwandishi Wetu, Dar es Salaam MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amesitisha kuendelea na zoezi la kuikodisha timu na nembo ya klabu hiyo na kuwaambia wasaidizi wake, wasitishe mipango yote ya maendeleo waliyokuwa wameanza kuifanya. Manji amewaambia wasaidizi wake kusitisha maandalizi ya Ligi ya Vijana ya Matawi ya Yanga, lakini amewaambia waandae siku rasmi ambayo atazungumza na vyombo vya habari na kuwaomba radhi Wanayanga ambao wamemuunga mkono muda wote. Yusuf Manji akiongea na wanahabari. Habari za uhakika ambazo Championi Jumatano limezipata, zinasema Manji alizungumza na wasaidizi wake jana mchana ikiwa ni dakika chache baada ya TFF kufanya mkutano na waandishi wa habari na kusema hawatambui suala la Yanga kuikodisha timu na nembo kwa Kampuni ya Yanga Yetu Ltd, kwa miaka 10. “Leo alionekana ni kama mtu aliyekata tamaa au asiyefurahishwa na jambo. Amewaita wasaidizi wake na wamefanya kikao, hakikuwa kirefu sana. “Amewaambia ameamu...