Posts

Showing posts from February 13, 2017

RC MAKONDA AKABIDHI ORODHA YA MAJINA 97 YA WAUZA DAWA YA KULEVYA KWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA JIJINI DAR LEO

Image
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akionyesha majina mengine 97 ya wauza Dawa za Kulevya awamu ya tatu kwa Bw. Rogers William Sianga kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ili yaanze kushughulikiwa.RC Makonda amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ya nne Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli, Katika mkutano uliofanyika kwenye ukubi wa Mwalimu Nyerere JNCC Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikabidhi majina mengine 97 kwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa Bw. Rogers William Sianga, kuwa ili yaanze kushughulikiwa.Rc Makond amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ya nne Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli. Mkuu w...

BREAKING NEWZ TID AOMBA RADHI KWA KUTUMIA ‘UNGA’, AWAPA NENO WANAOHOFIA ATAWATAJA

Image
Khaled Mohammed, maarufu kama Top In Dar es Salaam (TID), kwa mara ya kwanza amekiri hadharani kuwa alikuwa anatumia dawa za kulevya na kuwaomba radhi watanzania kwa ujumla. Akizungumza muda mfupi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja orodha ya awamu ya tatu ya wanaotuhumiwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya, TID amesema kuwa ameamua kuachana na dawa za kulevya na kwamba sasa anaunga mkono vita dhidi ya dawa hizo. “Nimesimama hapa kama kijana shupavu, mpambanaji na mwenye nguvu mpya. Lakini niko hapa mbele yenu kama mnyama, narudia tena mnyama… na niko tayari kuungana na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya,” amesema. “Unapaswa kuwa mnyama kama kaka yangu Makonda ili uweze kuishinda,” ameongeza. Ameongeza kuwa hakuna anayefahamu amepitia mangapi hadi kufikia hapo alipo leo na uamuzi wa kuacha dawa za kulevya akidai kuwa huenda ilihitajika nguvu ya dola kumsukuma...

Kajala Afunguka Kutomuona Wema Sepetu Selo

Image
Baada ya Miss Tanzania 2006/07 ambaye ni Mwigizaji wa Bongo Muvi, Wema Isaac Sepetu kusota lupango kwa siku kadhaa kufuatia kutajwa kwenye tuhuma za madawa ya kulevya na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, kabla ya kupandishwa mahakamani na kuachiwa kwa dhamana, staa mwenzake, Kajala Masanja ameibuka na kufunguka sababu ya kutokwenda kumuona mahabusu. Kajala, akiwa ni rafiki wa Wema, aliwahi kuokolewa kwenda jela na mrembo huyo baada ya kumlipia faini ya shilingi milioni 13, anadaiwa kutofika lupango katika Kituo Kikuu cha Polisi ‘Central’ jijini Dar alikokuwa ameshikiliwa Wema, jambo ambalo liliwashangaza wengi. Chanzo makini kililieleza Wikienda kuwa, kitendo cha kutokwenda kumuona wala kufika mahakamani siku aliyopandishwa kizimbani, kilimuumiza Wema na ndugu zake kwani hawakutegemea mtu kama Kajala angeshindwa kufika kumuona na kumsapoti shosti wake huyo. Katika mitandao ya kijamii, gumzo lilikuwa ni Kajala kutokwenda selo kumuona Wema hadi akatoka huku watu ...

HAWA NDIO WALIOTIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA MKOANI KILIMANJARO

Image
Baadhi ya watuhumiwa wa dawa za kulevya waliokamatwa katika msako uliofanyika kwa muda wa siku nne. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitaja majina ya watu wanadaiwa kujihusisha na usafirishaji,uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limetaja majina ya watu 47 wanaotuhumiwa kuhusika katika kusafirisha,kuuza na kutumia dawa za kulevya huku likifanikiwa kukamata misokoto 269 na miche 13 ya Bhangi,pamoja na kilogramu 32.9 za mirungi pia ikikamatwa. Kukamatwa kwa watuhumiwa hao pamoja na dawa hizo za kulevya kunatokana na msako mkali uliofanywa na kikosi maalumu cha jeshi hilo kwa muda wa siku nne katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro . Akitangaza majina hayo ofisini kwake ,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Mwanadamizi Msaidizi wa Polisi,Wibroad Mutafungwa alisema watuhumiwa ...