Posts

Showing posts from December 10, 2013

Waziri mkuu wa Thailand alivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema

Image
Waandamanaji wanaoipinga serikali wajilitokeza kwa wingi Jumatatu kumtaka waziri mkuu kujiuzu Waziri mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra ametangaza kwamba analivunja bunge na ataitisha uchaguzi wa mapema , "kwa haraka iwezekanavyo" kufuatia maandamano ya zaidi ya mwezi mmoja mjini Bankok kuipinga serikali yake. Katika hotuba kwa taifa Jumatatu asubuhi kiongozi huyo alisema atawaachia wananchi kuamua mustakbal wa nchi yao. Hata hivyo kiongozi wa chama cha upinzani cha Demokratic, Suthep Thaungsuban amesema hatositisha maandamano na wataendelea kuandamana hadi ofisi za Bi. Yingluck. Polisi waliripoti kwamba maelfu kwa maelfu ya watu waliandamana kuelekea makao makuu ya serikali siku ya Jumatatu asubuhi. Wabunge wa upinzani walijiuzulu Jumapili na kusema hawawezi kufanya kazi na bunge linalopingwa na wananchi. wamesema ingawa ameitisha uchaguzi lakini hawatosita hadi Bi Yingluck ameacha madaraka .

TUNA MUDA WA KUTOSHA KUJADILI MAISHA?ONGEA NA MWENZA WAKO

Image
NI  matumaini yangu kuwa wote ni wazima wa afya njema na mnaendelea vizuri na mihangaiko ya kila sikuya  maisha. Ni wakati mwingine tena tunakutana kujadili mambo yetu ya mapenzi na maisha. Leo nina jambo moja la msingi ambalo ningependa kujadili kwa pamoja, wakati huu tunapokaribia kumaliza mwaka na kuukaribisha mwaka mwingine. Najua wazazi wengi hiki ni kipindi cha maumivu kwa vile tutalazimika kutumia fedha kwa ajili ya kuandaa sherehe za Krismas na mwaka mpya. Lakini wakati tukishangilia kwa kuuona mwaka mpya 2014 kwa wale watakaojaaliwa, tutakutana tena na machungu ya maisha kwa sababu tutakuwa tunajipanga kuwapeleka watoto shuleni, ambao nao watachukua sehemu kubwa ya kipato kidogo kitakachobaki baada ya matumizi ya sikukuu. Mara nyingi tumekuwa tukijadili kuhusu mapenzi baina ya wanandoa na walio katika uhusiano, migogoro, adha, raha na karaha zake, lakini ni mara chache sana tumezungumzia juu ya watoto wetu, ambao ni muhimu mno kwetu pengine ...

Simulizi Za Mzee Madiba: Mandela ' Alipochacha Mfukoni' Akiwa Safarini.

Image
Na Maggid Mjengwa, Tunaendelea na simulizi hizi za Mzee wetu Madiba. Na hapa kuna bashraf ya tulikoishia asubuhi... "Mandela akajikuta amesimama miongoni mwa waheshimiwa na kukaribishwa chai. Na ghafla kukawa na foleni ya waheshimiwa wabunge mbele yake Mandela. Naye Mandela akashangazwa sana kuona wabunge wale wamejipanga mstari, na mmoja baada ya mwingine anakwenda mbele yake kumshika mkono na kumsalimu kwa heshima kubwa. Wakati tukio hilo likiendelea kumshangaza Mandela, basi, ilipofika zamu ya Mbunge wa tatu kwenye mstari kumsalimu Mandela akasikia sauti ikimtamkia kutoka kwa Mbunge huyo; " It is a great honour to shake the hand of the reverend Chief Luthuli, winner of the Nobel Peace Prize." ( Nelson Mandela, Long Walk To Freedom, pg. 357.) Kwamba mbunge huyo alitamka kuwa ilikuwa heshima kubwa kwake kushikana mikono na Chifu Luthuli, mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobeli. Ndipo hapo Mandela akafahamu, kuwa Karani yule wa Bunge alichanganya mambo! .. En...

INASIKITISHA SANA: KICHANGA CHAKUTWA KIMEKUFA IRINGA BAADA YA KUTUPWA NA MTU ASIYEJULIKANA

Image
Na. LEWIS MBONDE BLOG,IRINGA Tukio hili limetokea hapa mkoani Iringa asubuhi ya leo katika eneo la samora karibu na mashine ya kukamua mafuta ya alizeti kichanga kimekutwa kimekufa baada ya kutupwa.Shuhuda wa tukio hilo ni mwenye nyumba ambaye alikua anafanya usafi wa mazingira na kukuta kanga ikiwa imevilingisha huyo mtoto anae kadiliwa kua na miezi 8.Maiti hiyo ya kichanga ikaondoka na polisi.mpaka sasa muhusika hajapatikana.

SHAA AKIRI KUTEMBEA NA MASTER JAY ... AANIKA SIRI ZAO NZITO NZITO

Image
Akihojiwa katika kipindi cha ng'ari ng'ari, Shaa alisema," mimi sikuwa  sababu ya kuachana kwa wao wawili (master jay na mama watoto wake),kwani  ugomvi au kuachana kwa watu wawili huwa inahusu wao wenyewe wawili ila  sio mtu watatu, na kwakuwa mimi nilikuwa nimetoka kutendwa ilichukua  muda kidogo hadi kuja kuwa na mahusiano na Master Jay hata yeye pia  aliniambia alikuwa na maumivu yake ndio mana ilichukua muda hadi kuwa na  mahusiano. Hivyo kwanini niachie bahati yangu, Nampenda sana Master" Mtangazaji: Huwa unapika ukiwa nyumbani, ili kumpagawisha mzee Shaa: Nashukuru sana kwani Master anapenda sana kupika kwakweli   na mara nyingi huwa anapika yeye kuliko mimi, na Inshalah namshukuru  sana Mwenyezi Mungu

Picha 9 za birthday party ya Nicki Minaj…hiyo keki yake sasa.

Image
  First lady wa label ya YMCMB Nicki Minaj amesherekea birthday yake akitimiza miaka 31 na mafanikio ya kujivunia kwenye kazi yake ya muziki. Party hiyo ikifanyika huko L.A na restaurant nzima ilibadilika rangi yake na kuwa ya pink maalum kwa ajili ya party ya Minaj ambayo ilihudhuliwa na Lil Twist,Safaree boyfriend wa Nicki Minaj na watu wengine. Nicki aliletewa keki mbalimbali pamoja na stripper pole maalum kwa ajili ya party hiyo.

Makubwa haya ... Wanaume wawili wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wapata vyeo vikubwa serikali, mmoja awa waziri mkuu na mwingine awa makamo waziri mkuu.

Image
 Xavier Bettel na Etienne Schneider Hii itakua ya kwanza duniani kwa wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kupata vyeo vikubwa kwenye serikali kuu ya nchi. Makundi mengi yenye maoni tofauti yamekuwa yakipinga mapenzi ya jinsia moja na makundi mengine yakitetea, huko Luxemburg mwanaume anayejulikana kwa jina Xavier Bettel ambaye ameweka wazi kwamba anashiriki mapenzi ya jinsia moja amekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo. Hapo hapo mwanaume mwingine Etienne Schneider ambaye pia aliweka wazi kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja amepewa umakamo waziri mkuu akimsaidia kazi Xavier Bettel . Baada ya wawili hawa kupata vyeo hivi vya juu imefanya nchi ya Luxemburg kuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na viongozi wa juu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja waziwazi. Waziri mkuu kulia na kushoto ni boyfriend wake.

STARS DHIDI YA KENYA ‘INAYOBEBWA VIBAYA’ NA MAREFA CHALLENGE 2013, PATACHIMBIKA MACHAKOS LEO

Image
Mungu Ibariki Tanzania: Kikosi cha Stars Challenge 2013 na chini ni Harambee....na "Washindwe". Na Mahmoud Zubeiry, Machakos TANZANIA Bara 'Kilimanjaro Stars', leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos, kumenyana na wenyeji, Kenya 'Harambee Stars' katika Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kuanzia saa 7:00 mchana. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Stars chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen kufika Nusu Fainali ya michuano hiyo, baada ya mwaka jana pia mjini Kampala, Uganda ambako ilitolewa na wenyeji, Uganda 'The Cranes' kwa kufungwa mabao 3-0 Lakini Kim, amelipa kisasi kwa The Cranes, baada ya Stars kuivua ubingwa Uganda Jumamosi kwa kuitoa kwenye Robo Fainali, Uwanja wa County ya Mombasa, zamani Manispaa kwa penalti 3-2, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90. Baada ya kumaliza shughuli hiyo pevu, Kim anakabiliwa na jukumu lingine zito mbele yake, ambalo ni Nusu Fainal...

Msanii mkubwa wa hiphop kutoka Marekani ajichora tatoo kubwa ya Nelson Mandela

Image
Hakuna mtu yoyote ambaye hajaguswa na kifo cha Mzee Nelson Mandela kutokana na historia ya pekee aliyoiacha kiongozi huyu wa Afrika Kusini. Kuanzia mataifa ya Asia,Ulaya,Marekani, wanamichezo,waigizaji hadi watu wa kawaida wameonyesha masikitiko yao kwa kumpoteza mfano mzuri kwenye uongozi. Headline mpya inamhusisha msanii nguli wa hiphop The Game ambaye ni mpenzi mkubwa wa tatoo. Hivi sasa amechora tatoo kubwa za sura za wanae,Barack Obama, Trayvon Martin na Nelson Mandela akiangalia nje ya gereza. The game ali-share picha akionyesha tatoo hiyo kubwa na kuandika ,“The finished ‘Nelson Mandela’ lookin out of the prison bars by @NikkoHurtado done on my side. 7 hour sitting…. Few more hours to tie in the tats around it & we solid,”.

HAYA HAPA MAAJABU 10 YA MSIBA WA MANDELA

Image
RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela, mweusi wa kwanza kushika wadhifa huo katika taifa lenye uwezo mkubwa kiuchumi na kijeshi barani Afrika, alifariki dunia Alhamisi iliyopita akiwa nyumbani kwake jijini Johannesburg. Nelson Mandela. Kifo chake kimeushtua ulimwengu na kwa mara ya kwanza katika historia, dunia nzima imesimama nyuma ya jemedari huyo, kila mmoja akionesha masikitiko yake. Wakati dunia ikisubiri mazishi yake ambayo pia yatavunja rekodi ya mazishi yote yaliyowahi kufanywa tokea kuumbwa kwa uso wa dunia hapo Desemba 15 mwaka huu, Uwazi limebaini maajabu kumi yanayoambatana na msiba huo. AIR FORCE ONE KUBEBA MARAIS WATANO WA MAREKANI AIR Force One ni ndege inayombeba Rais wa Marekani aliye madarakani na kumpeleka popote duniani. Lakini katika hali ya kushangaza, Idara ya Usalama ya Marekani imetoa ruhusa kwa marais wastaafu wakiwa na wake zao, kuandamana na Rais Barak Obama kuhudhuria mazishi ya shujaa huyo wa dunia. Hii ni mara...

RAIS KIKWETE AWASILI PRETORIA KUHUDHURIA IBADA KUU (MEMORIAL SERVICE)YA MSIBA WA MANDELA

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku wa kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela. PICHA NA IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili katika mji mkuu wa Afrika Kusini wa Pretoria usiku wa leo, Jumatatu, Desemba 9, 2013, kuhudhuria Ibada Kuu ya Kitaifa (Memorial Service) ya msiba wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg. Rais Kikwete anajiunga na mamia ya viongozi wa nchi mbali mbali duniani kuomboleza kifo cha mmoja wa viongozi mashuhuri zaidi duniani katika karne za 20 na 21. Rais Kikwete ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa Pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na mkewe Mama Asha; Mama Salma Kikwete na Ndugu Abdulahramani Kinana, Katibu wa Mkuu wa CCM

Jinsi KIGOMA ALL STARS a.k.a Lekadutikite walivyoiteka Mombasa

Image
  . Kundi la Kigoma all stars limeanza ile tour ya East Africa kutembelea nchi kama Kenya, Rwanda na Burundi kwa ajili ya kutangaza Amani kwa muziki wao. Wameianza tour tayari kwenye jiji la Mombasa. Hizi ni baadhi tu ya picha za tukio lenyewe. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .