Posts

Showing posts from May 25, 2016

Waziri Mkuu Akutana na Watanzania Waishio Zambia

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio Zambia kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka Mei 24, 2016. Majaliwa alikwenda Zambia kumwakilisha  Rais John Magufuli kwenye Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi. Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka.  Majaliwa  alikwenda Zambia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye  mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016. Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka.  Majaliwa  alikwenda Zambia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye  mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016. Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri...

Boti yapotea Ziwa Nyasa...Watu Kadhaa Wahofiwa Kufa.

Image
WATU kadhaa wanahofiwa kufa maji baada ya boti iliyokuwa ikifanya safari kutoka Mbamba Bay nchini Tanzania kwenda Nkhata Bay Malawi kuzama Ziwa Nyas na boti kutoweka. Duru  za usalama zinasema Boti hiyo haijulikani ilipo wala abiria waliokuwemo ndani yake jambo ambalo limezua sintofahamu kubwa, huku wakihofia kuzama. Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, kusini mwa Tanzania, Zuberi Mwombeji alisema haifahamiki ajali hiyo ilitokea aneo gani la Ziwa lakini juhudi za kuitafuta zinaendelea. “…Usafiri wa kutoka Mbamba Bay mpaka Nkhata Bay huchukua saa tano mpaka sita, walipoona Nkhata Bay hawajafika waliwasiliana na watu wa Mbamba Bay ndipo ilipojulikana kuwa kuna tatizo limetokea,” alisema Kamanda Mwombeji. Chanzo cha ajali hiyo kinaaminika ni hali mbaya ya hewa ziwani, hali inayoaminika kuwa ilisababisha Boti hiyo kupigwa dhoruba. Hata hivyo taarifa zinasema boti hiyo ikiwa njiani ilianza kuingiza maji ndipo juhudi za kuyatoa ndani ya boti zilianza kabla ya kuzidi...

Baada ya Jackline Wolper kuwa na Harmonize, kataja jina analomuita Diamond kwa sasa.

Image
Kwa sasa headlines nyingi katika upande wa mastaa Tanzania ni stori kuhusu penzi la muigizaji Jackline Wolper na msanii wa Bongo fleva kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) Harmonize ndio Topic kubwa town. Katika mahojiano na Take One ya Clouds TV  na Zamaradi Mketema , Jackline Wolper ameeleza mambo kadhaa kuhusiana na penzi lake la Harmonize , Diamond ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake anachukuliaje mahusiano yao? “Diamond rafiki yangu sana ni mtu ambae nategemea hata kuja kufanya nae filamu, Diamondi ni rafiki yangu sana licha ya watu wanaweza wasielewe, lakini sasa hivi Diamond ni baba mkwe wangu, “kuhusu Harmonize nampenda kwa sababu ana hofu ya mungu, ana heshima sana mwisho hawezi kufanya maamuzi bila kuomba ushauri, katika kunipenda mimi alipiatia pia kuomba ushauri kwa Diamond ambaye ni boss wake kaka yake na kupewa ruhusa kwa hiyo Baraka zimetoka kwa Diamond mwenyewe”

DIVA ASEMA ANATAKA KUZAA MTOTO MMOJA TU AFUNGE KIZAZI

Image
Star wa Clouds FM, Diva, amefunguka na amesema kwenye maisha yake anataka azae Mtoto Mmoja tu wa Kiume na kufunga Kizazi baada ya hapo. Akiongea na Makorokocho, Diva amesema amekuwa akisumbuliwa na Maumivu ya Tumbo toka anakuwa binti na imefikia kipindi analazwa kwa siku 1 au 2 toka anasoma ili apate matibabu akiwa karibu na madaktari sababu wakati anasoma alikuwa anafika stage anazimia maumivu hayo yakizidi lakini baada ya kuwa mkubwa yakaanza kupungua. Mwaka jana, 2015, Diva alifanyiwa operesheni katika hospital ya Sanitas na ushauri alioambiwa ni akae kidogo halafu azae. Na sasa star uyo amefunguka na kusema atazaa Mtoto Mmoja tu na anaombea awe wa Kiume na baada ya hapo atafunga kizazi. "Naogopa sana kubeba mimba na kuzaa, so wil do that Mara Moja tu Kwa Miezi 9 then after that Ntafunga kizazi na Mtoto wangu nitaenda jifungulia nchi za Marekani ili apate uraia wa huko" Alisema Diva.

MTOTO WA KABWE AMCHUNIA MAKONDA

Image
Siku ya jana ilikua ni siku ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Ndg. Wilson Kabwe iliyofanyika viwanja vya Karimjee katikati ya Jiji la Dar es salaam. Katika hali ya kutoelewa nini kinachoendelea, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alijikuta akiganda kwa sekunde kadhaa mbele ya binti wa marehemu Wilson Kabwe anayefahamika kwanjina la Anna pale alipo jaribu kumpa mkono wa pole lakini binti huyo alikataa kujibu huku akibubujikwa na machozi ya uchungu. Habari kutoka kwa watu karibu wa familia zinasema binti huyo alifanya hivyo kutokana na machungu aliyokuwa nayo juu ya Makonda ambae wiki za usoni inaeleweka ya kwamba Mkuu huyo wa mkoa alikuwa mstari wa mbele kuchochea moto ambao ulisababisha Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo . Habari za ndani zinasema kitendo hicho cha binti huyo cha kukataa mkono wa Makonda kimetokana na hotuba aliyotoa Mh. Makonda ambayo kwa maudhui ilikua im...