Posts

Showing posts from May 24, 2016

Mamia Wauaga Mwili wa Kabwe Dar

Image
         Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akipita mbele ya jeneza. Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda (kulia) akimpa pole mke wa Marehemu Kabwe aitwaye Faith Kabwe. Viongozi mbalimbali wakipita mbele ya jeneza kutoa heshima za mwisho. Mwanasiasa mkongwe hapa nchini, Kingunge Ngombale Mwiru (kulia) akipita mbele ya jeneza. Waombolezaji wakiendelea kutoa heshima za mwisho. Mamia ya waombolezaji wakiwa katika mstari kutoa heshima zao. Walioko mbele ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, Waziri George Simbachawene, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi. Waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Karimjee Dar. Mke wa marehemu Kabwe, Faith Kabwe (wa kwanza kulia) akiongozana na wanafamilia walipofika viwanja vya Karimjee. Jenez...

TAKUKURU WAZINDUA KAMPENI YA LONGA NASI JIJINI DAR LEO.

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba kuashiria uzinduzi wa gari la matangazo ya Kampeni ya kupambana na Rushwa ya LONGA NASI kwa kupiga namba 113 na kutuma kutuma sms kwenda namba 113 ili kutoa taarifa ya kutoa au kupokea Rushwa kwa TAKUKURU. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za watu wanaotoa rushwa au kupokea rushwa kwaajili ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 unayoweza kupiga na kutuma sms za kawaida  Uzinduzi huo umefanyika leo  katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam. Mkuu wa Kitengo cha Tehama TAKUKURU, Neema  Mwalyelye akitoa maelekezo kwa  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipot...

Tamko la Madiwani Misungwi: Kitwanga Hakulewa Kama Ilivyopotoshwa.

Image
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga. UTANGULIZI Ndugu Waandishi wa habari, Karibuni kwenye mkutano huu mfupi ambao lengo lake ni kutoa taarifa yetu fupi kuhusu ukweli uliojificha kuhusu kitendo kilichopelekea Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga. Tunaamini kwa uwezo mliona kama waandishi wa habari, taarifa hii itafikia umma wa Watanzania kama ilivyokusudiwa. UFAFANUZI Kama mnakumbuka mnamo tarehe 20 Mei mwaka huu, Rais Dk John Pombe Magufuli alichukuwa uamuzi wa kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga ambaye pia ni Mbunge wa Misungwi kwa kosa la kwamba Mhe. Kitwanga aliingia bungeni akiwa amelewa. Sisi wananchi wa Jimbo la Misungwi tumesikitishwa sana na taarifa na uamuzi huu kwa kuwa tunaamini kuwa kuna dhamira iliyojifika iliyopelekea Mhe Rais kufanya maamuzi haya. Ukweli ni kwamba huu ulikuwa mpango wenye dhamira ovu na uliogubikwa na uongo mwingi uki...

Wakili Hashim Rungwe Aishauri Serikali Mambo Mazito

Image
Wakili Hashim Spunda. MMOJA wa wagombea Urais na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Umma (Chauma), Wakili Hashim Spunda Rungwe amefanya mahojiano maalum na wahariri wetu ili kutoa tathmini yake ya utawala wa miezi sita wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli tangu ashike madaraka ya kuongoza nchi. *Azungumzia mbinu ya kupunguza bei ya sukari, asema watu wana njaa! Wakili Rungwe ameshauri mambo mazito ya nini cha kufanya ili nchi iweze kusonga mbele kimaendeleo. Hata hivyo, ametoa maoni juu ya mjadala wa Bunge kutooneshwa laivu na sakata la sukari, fuatana nasi katika makala haya ujue kile alichokisema: Tupe maoni yako kuhusu utawala wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ambaye amefikisha miezi sita akiwa madarakani, je, anakwenda vizuri? Rungwe: Miezi sita ya Serikali ya Awamu ya Tano sijasikia mpango wowote wa kuondoa njaa kwa wananchi. Lazima rais ajue kwamba watu wana njaa na zifanyike juhudi kuhakikisha kipato kwa mwananchi mmojammoja kinaon...

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 24.05.2016

Image