UNYAMA Dar! Mke wa Mtu Atembezwa MTUPU, Apigwa Mawe na Kuchomwa Moto!
Kundi la vijana hao wakimtembeza Shakila mitaani huku akiwa mtupu. Na Makongoro Oging’ DUNIA katili! Mrembo mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shakila Kocho (21), mkazi wa Tabata- Kimanga jijini Dar amelazwa Wadi namba 24, Jengo la Mwaisela, Hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia majeraha yaliyotokana na kupigwa mawe na kuchomwa moto wa petroli kwa kisa cha tuhuma za kuwa kwenye mtandao wa wizi wa bodaboda. Wakimshambulia kwa mawe. WALIOTEKELEZA UKATILI Msichana huyo alifanyiwa kitendo hicho hivi karibuni maeneo ya Buguruni Sukita, Dar na watu wanaodaiwa kuwa ni madereva wa bodaboda ambao ndiyo waliomtuhumu. Taarifa zilizopatikana kwa mashuhuda zinadai kwamba, Shakila kabla ya kuchomwa moto alitembezwa mtupu mtaani huku watu wakimsonga na baadaye akapigwa mawe na fimbo halafu akamiminiwa petroli na kulipuliwa kwa kiberiti. Shakila akiwa ameanguka. MSOMALI ASAIDIA Kwa mujibu wa mashuhuda hao, wakati Shakila akiwa chini kutetea roho yake huku akiungua moto, mwanaum...