Posts

Showing posts from November 19, 2013

"Niliokoka kufa kutokana na miujiza ya mungu"..Ufoo Saro

Image
Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro ambaye alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi, amefanya ibada na kusema: ā€œNamshukuru Mungu kwa kumponya.ā€ Ni mara ya kwanza Saro kuzungumza tukio hilo tangu aliporuhusiwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu, MOI ya Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa. Katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibamba, Jimbo la Magharibi, Ufoo huku akitokwa na machozi na wakati mwingine kushindwa kuzungumza alisema: ā€œNi miujiza tu ya Mungu yeye kunifanya mimi kuwa hai leo.ā€ Mtangazaji huyo ambaye alilazwa kwa zaidi ya wiki mbili, aliwashukuru watu wote waliomtia moyo, kumsaidia kipindi chote alichokuwa mgonjwa. ā€œSina cha kuwalipa, ninawashukuru sana kwa wema wenu, pia kwa kuniombea. Mungu ni mkubwa na amenipigania, naendelea vizuri kwa sasa,ā€ alisema na kuongeza: ā€œMungu alinisimamia na nyinyi pia mliniombea, hakika sina budi kushukur...