Posts

Showing posts from July 26, 2018

Katibu Tawala Mkoa Mtwara wa Awaasa Maafisa Habari Kutekeleza Majukumu Yao Kwa Weledi

Image
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Alfred Luanda akisisitiza jambo kwa  Mwakililishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo wakati wa ziara iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO katika Mkoa wa Mtwara leo kuona utendaji wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini pamoja na changamoto zilizopo ili kuweka mikakati ya pamoja ya  kuzitatua hali itakayoimarisha Mawasiliano Serikali kwa umma katika mkoa huo. kurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara  Bw. Omari Kipanga akisisitiza jambo wakati wa ziara iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO katika Mkoa wa Mtwara leo kuona utendaji wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini pamoja na changamoto zilizopo ili kuweka mikakati ya pamoja ya  kuziondoa hali itakayoimarisha Mawasiliano Serikali kwa umma katika Halmashuri hiyo

HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI YAJIDHATITI KUIMARISHA MAWASILIANO NA WANANCHI

Image
Kiongozi wa ujumbe kutoka Chama cha maafisa Habari na Mawasiliano  Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO  Bi. Gaudensia  Simwanza akisisistiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi.  Changwa Mkwazu      wakati wa ziara ya ujumbe huo katika halmashauri hiyo uliolenga kuona utendaji kazi wa Maafisa  Habari na Mawasiliano na namna wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali ili kuweza kuisemea Serikali kimkakati. Kiongozi wa ujumbe kutoka Chama cha maafisa Habari na Mawasiliano  Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO Bi. Gaudensia Simwanza akisisitiza jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wa Halmashuri ya Wilaya ya Masasi Bi mara baada ya ziara ya ujumbe huo katika Halmashuri hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya  ujumbe  wa viongozi wa Chama cha maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Ha

Nyumba mbili zachomwa Moto Mwanza kisa wizi

Image
Na Paschal D.Lucas, Mwanza Wananchi waliojichukulia sheria mkono wamechoma nyumba mbili za familia moja na nyingine kuziharibu katika mtaa wa Nyakabungo "A" kata ya Isamilo wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza  baada ya kuona watoto wa familia zile wanajihusisha na uhalifu hapo mtaani hapo mara kwa mara. Maamuzi hayo yamekuja baada ya wananchi kudai kuwa watoto hao wamekuwa wakikamatwa na kupelekwa mahakamani kushitakiwa lakini mara nyingi wamekuwa wakiachiwa kwa dhamana na kurudi mtaani kuendelea tena na tabia hiyo kitendo ambacho kimekuwa ni kero kubwa  kwa wananchi wa eneo hilo. Tukio hilo lilitokea majira ya saa 3 usiku wa tarehe 25,Julai 2018 ambapo katika tukio hilo nyumba mbili zilizoharibiwa ni mali ya Selina Francis (50) na Abdallah Mwita wote wakiwa ni wakazi wa Nyakabungo mkoani humo. Vile vile nyumba moja mali ya Manka Francis James iliharibiwa vibaya na kundi hilo kwa kuvunjwa milango na madirisha na kuharibu vitu mbalimbali vilivyokuwemo ndan

Tambwe Afunguka Mazito Yanga

Image
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameibuka na kusema wanaumizwa na hali inayoendelea katika timu hiyo lakini haiwafanyi washindwe kupigana huku wakiwaomba mashabiki kuwa kitu kimoja kabla ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. Yanga inatarajiwa kurudiana na Gor Mahia Jumapili ya wiki katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar baada ya ku­fungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Kenya. Akizungumza na Championi Jumatano , Tambwe alisema kwa sasa bado wanapita katika kipindi kigumu lakini hawezi kuwafanya washindwe kufanya vizuri katika mchezo huo wa maru­diano huku akiwaomba mashabiki wasichoke kuwasapoti. “Tunajua matokeo hayakuwa mazuri kwetu katika mchezo wa kwanza kwa sababu hakuna ambaye alitege­mea tutapoteza tena kwa idadi kubwa ya mabao lakini kwa kuwa wenzetu walitumia mapungufu yetu kupata ma­tokeo. “Nadhani huu ni wakati wa kuende­lea kushikamana, mashabiki wetu hawa­paswi kuendelea kuka

Mbelgiji Aanza Kukiunga Kikosi Upya

Image
KOCHA Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ameanza kutoa mafunzo ya mfumo anaotaka kuutumia katika msimu wa 2018/19 akiwa na Simba. Simba imeweka kambi ka­tika mji mdogo wa Kartepe ambao uko mlimani kabisa, sehemu maalum kwa ajili ya kambi za timu. Aussems ameanza kukinoa kikosi chache akiwafundisha mifumo na namna ya uchezaji katika masuala mbalimbali. Kocha huyo amekuwa aki­waonyesha wachezaji wake namna ya kulinda lakini pia kushambulia kwa tahadhari. Wakati Simba ilipotua hapa, kocha huyo alianza kutoa mafunzo ya kawaida, zaidi wachezaji wakioneka­na kupasha misuli kawaida. Inaonekana ame­kuwa akiongeza mazoezi taratibu huku akichanganya na aina ya uche­zaji. Makocha wengi huanza kufundisha mifumo baada ya timu zao kupata mazoezi ya kuto­sha. Lakini Mbelgiji huyo anaonekana kuwa tofauti ki­dogo akienda anachangan­ya mazoezi ya kawaida na mifumo, taratibu.

Beki Simba atua Singida United kwa mkopo

Image
Klabu ya soka ya Singida United imethibitisha kuwa imemsajili mchezaji Jamaly Mwambeleko kutoka Simba kwa usajili kamili tofauti na taarifa zilizoeleza kuwa wamemchukua kwa mkopo, huku wakiweka wazi kuwa wamemwongeza mwaka mmoja na sasa ni mchezaji wao kwa miaka miwili. Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga ameeleza kuwa walifanya mazungumzo na Simba na kumalizana nao kisha kumpa mkataba wa mwaka mmoja Jamaly Mwambeleko lakini baadae walimwongeza mwaka mmoja na kuwa miwili. ''Tumemsajili Mwambeleko kwa usajili kamili wala hajaja kwetu kwa mkopo, ila awali mazungumzo yalikuwa hivyo lakini kocha Hemed Morocco akapendekeza tuwe naye kwa muda mrefu ndio akasaini mkataba wa kuitumikia Singida United kwa miaka miwili'', - amesema. Jamaly Mwambeleko ambaye anacheza nafasi ya mlinzi wa kushoto ni sehemu ya wachezaji walioachwa na Simba katika usajili huu kwa kile kilichoelezwa ni kutokuwa na nafasi ya kucheza hususani nafasi yake pale Simba kuwa na w

Jafo azitaka halmashauri kutoweka riba mikopo ya wajasiriamali

Image
Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo amezitaka halmashauri za miji na majiji kutoweka riba katika fedha za mikopo zinatolewa kwa ajili ya vikundi vya wajasiriamali hapa nchini. Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 950 zilizotolewa na jiji la Dodoma kwa wajasiliamali, Mheshimiwa Jafo amesema serikali ya awamu ya tano inalenga kuwawezesha watanzania hivyo haikubali wananchi kutozwa riba. Akizungumza katika tukio hilo, naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera,bunge,ajira kazi vijana na watu wenye ulemavu Mhe. Anthony Mavunde amesema jiji la Dodoma ni kati ya halmashauri chache nchini zilizoweza kutimiza sheria ya kuhakikisha linatoa mikopo kwa vikundi vya kina mama,vijana na watu wenye ulemavu ili Kuwawezesha kuondokana na umaskini. Akielezea kuhusu fedha hizo, mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Godwin Kunambi amesema jiji la Dodoma limevuka malengo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka

KINDA WA LEICESTER CITY AITWA SERENGETI BOYS KUCHEZA MICHUANO YA CECAFA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemualika mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Leicester City ya England, Anthony Starkie kuja kujiunga na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys. Taarifa ya TFF usiku wa Jumatano imesema kwamba Starkie anatarajiwa kuwasili Alhamisi mjini Dar es Salaam baada ya kuruhusiwa na Leicester City, mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya wakubwa England. Atajiunga na Serengeti Boys ambayo inajiandaa kushiriki michuano maalum ya vijana Afrika Mashariki na Katik ijulikanayo kama CECAFA Zonal Qualification. Wazi uamuzi wa TFF kumuita kijana huyo unafuatia agizo la Mkurugenzi wa Michezo, Dk. Yusuphu Singo kwamba wafuatilie vipaji vya wachezaji wa Kitanzania wanaocheza nje. Singo alitoa kauli hiyo kufuatia mshambuliaji Yussuf Yurary Poulsen, anayezaliwa na baba kutoka Tanga  kuichezea Denmark, nchi ya mama yake kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu nchini U

Makamu wa Rais aahidi Serikali kutatua changamoto ya barabara Mbeya

Image
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wakazi wa Mkoa wa Mbeya kwamba serikali imejipanga kutekeleza na kutatua changamoto muhimu za kimaendeleo, ikiwemo ya miundombinu ya barabara. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati akizungumza na mamia ya wananchi katika eneo la Mbalizi Wilayani Mbeya eneo linalotajwa kuongoza kwa matukio ya ajali za barabarani.  Amesema, katika kulitekeleza hilo, tayari serikali imeshughulikia changamoto ya ujenzi wa barabara ya mchepuko ya kilomita 40 ambayo itasaidia kupunguza au kudhibiti ajali za barabarani zinazotokea kwenye barabara kuu ya Tanzania na Zambia (TAZAMA).  “Mwaka juzi mlifanya kazi kubwa sana, tumekuja kuwahikikishia kwamba serikali itatekeleza yale yote tuliyo ahidi, nadhani spidi mnaiona,”amesema. Mama Samia pia amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani kwani ndio sialaha ya maendeleo na kuwasisitiza kuchaguai viongozi watakaoendana na kasi ya rais na waioendekeza tama wakati wa uchaguzi wa viongozi