Breaking News: Polisi Yakanusa DCI, Mambosasa Kuondolewa
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa. MSEMAJI wa Jeshi la Polisi nchini, Barnabas Mwakalukwa, amekanusha taarifa zinazozagaa mitandaoni zinazohusu jeshi la polisi kufanya mabadiliko na kuomba wananchi kuzipuuza. Taarifa ya msemaji hiyo imeeleza kuwa mkuu wa jeshi hilo, IGP Simon Sirro, amewataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo zenye lengo la kupotosha umma na kuwataka kuacha kutumia mitandao ya kijamii na badala yake waitumie kupeana taarifa za kuleta maendeleo. “Serikali na vyombo vyake ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa umma,” ilisema taarifa ya Mwakalukwa. Taarifa ambazo si za kweli zilidai Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, wamepangiwa majukumu mengine. Ziliongeza kusema kuwa Mambosasa amerejeshwa makao makuu kwenye kamisheni ya ushirikishwaji jamii, na Charles Kenyela amekuwa DCI mpya huku Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi, ...