BREAKING NEWS: Lissu Awaongoza Mawakili Kugoma Kuingia Mahakamani
Tundu Lissu akiakiwa na mawakili wengine wakati wakizungumza na wanahabari katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dar. RAIS wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Tundu Lissu amewaongoza mawakili nchini kugoma kuingia mahakamani kwa muda wa siku mbili Agosti 29 na 30, 2017 wakilaani tukio la kushambuliwa kwa ofisi za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA Advocates iliyolipuliwa kwa bomu usiku wa kumakia Jumamosi iliyopita. “Mengi wamefanyiwa mawakili lakini hili la juzi tumesema hatukubali kukaa kimya wakati mawakili wetu wanashambuliwa. Kwa busara za TLS tuliona tufanye maamuzi ya kusimamisha kazi kwa siku mbili ili kupeleka ujumbe kuwa jambo hilo si jema,” alisema Lissu. Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Dr. Hellen Kijo Bisimba akizungumza na wanahabari . Kuhusu endapo mawakili wote wamegoma Lissu alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa, hadi jioni ambapo ripoti kamili itakuwa imepatikana kwa kuwa kuna mawakili wengine walikuwa na kesi as...