Posts

Showing posts from June 11, 2016

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AONGOZA MATEMBEZI YA WAFANYAKAZI WA BENKI KUU.

Image
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wasanii wa Benki Kuu baada ya kuongoza matembezi  kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.  Zaidi ya shilingi milioni263 zilichangwa. Bendi ya Poli ikiongoza matembezi  ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.Zaidi ya shilingi263 milioni zilichangwa.    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza matembezi ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu ha viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu, Benno Ndulu na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Mako...

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI

Image
Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.   Mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.  

Wawili wawachinja wake zao, mwingine amuua mama yake!

Image
Matukio ya Dodoma Samson Joramu(44), mkazi wa Chololo, Kata ya Kikombo, alimchinja mke wake, Rehema Joram (43) kabla ya kujiua kwa kunyonga katika shamba lake. Watu walioshuhudia walisema, Joramu baada ya kumuua mkewe alijinyonga na aliandika ujumbe uliokutwa mfukoni kwake, ukisomeka: “Mama tunza wanangu, mimi nimekufa.” Kadhalika aliandika orodha ya watu anaowadai. Katika tukio jingine, Amos Kalenda, mkazi wa Kikombo, Dodoma anadaiwa kumuua mama yake mzazi, Joyce Kalenda kwa kumchinja. Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa ni mama huyo kumnyima chakula. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa akizungumzia tukio hilo alisema kuwa: “Ni kweli taarifa za vifo kutoka Kikombo ninazo, yule mmoja alimuua mama yake kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili jana (juzi), na huyu mwingine alimuua mke wake asubuhi ya leo (jana) kisha naye akajinyonga,” alisema. Tukio la Tarime Mkoani Mara katika Wilaya ya Tarime, Wambura Mariba (50) mkazi wa Matongo, Nyamongo, T...

ANGALIA PICHA ZA SHEREHE UFUNGUZI WA MICHUANO YA EURO 2016

Image
Michuano ya UEFA Euro 2016 ilianza rasmi kufanyika Ufaransa usiku wa June 10 2016 kwa kupigwa mchezo kati ya Ufaransa dhidi ya Romania, kabla ya kuanza kwa mchezo huo kulifanyika sherehe mbalimbali za kuashiria usiznduzi wa michuano hiyo. Wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo kulikuwa na burudani mbalimbali ikiwemo perfomance za muimbani Zara Larsson na David Guetta walikuwepo pia kuburudisha watu katika michuano hiyo kwa mwaka 2016.

RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA BALOZI WA OMAN ANAYEMALIZA MUDA WAKE HAPA NCHINI.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda wake wa kufanyakazi hapa nchini.