Hatimaye sababu za Wema Sepetu na Diamond kurudiana zajulikana, soma mchezo mzima ulivyokuwa!
Baada ya kimya kirefu juu ya tetesi za kurudiana kwa mwanadada Wema Sepetu na Diamond kuzagaa kwenye mitandao hasa baada ya picha za wawili hao waliokuwa wamechana kuonekana wakila “bata” pamoja maeneo ya Hong Kong huko kwenye bara la Asia, sababu na ukweli wa namna wawili hao walivyorudiana umewekwa waza baada ya hivi karibuni msanii diamond platnumz kuzungumza na mtandao wa GPL na kuelezea jinsi tukio hilo zima lilivyokuwa. Katika mazungumzo hayo Diamond alitaja mambo haya makuu matano yaliyosababisha mpaka aamue kurudisha vikosi kwa mwanadada Sepetu. Sababu ya kwanza (1) – UKARIMU WA WEMA Diamond alisema kuwa alipotua Hong Kong alishangaa kukutana na mapokezi ya Wema kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo hakulitegemea. “Alinionesha ukarimu wa hali ya juu mno. Wakati tulipokuwa hapa Bongo tulikuwa hatusalimiani. “Kuna vitu vingi vya ajabu vilitokea huko nyuma kati yangu na Wema. Sikufikiria wala kuwaza kama anaweza akawa mkarimu kwangu kiasi kile. A...