Posts

Showing posts from November 2, 2016

Waendesha Bajaji Wenye Ulemavu Wafunga Barabara Dar

Image
Dar es Salaam: Waendesha Bajaji wenye ulemavu wanaofanya shughuli zao katika Jiji la Dar es Salaam wamelazimika kufunga barabara ya Mission na kuzuia magari kuingia katika ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala. Wamefanya hivyo kwa lengo la kushinikiza wapewe vituo maalum vya kupakia na kushusha Abiria katikati ya jiji. Tupia Comm

Picha: Thomas Mashali Alivyozikwa Jijini Dar Leo

Image
Hatimaye mwili wa bondia Thomas Mashali umezikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar mchana huu. Picha zote na Boniphace Ngumije / GPL

MBUNGE Godbless Lema ALETA HALI TETE BUNGENI…Adai Waziri Alimshauri Wafanye Fujo Arusha ili Aingilie

Image
GODBLESS Lema, Mbunge wa Arusha Mjini amesema kwamba, alishauriwa na George Simbachawene, Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa, amfungie ofisini Athumani Kihamia, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ili kuibua vurugu na kisha (Simbachawene) aingilie, anaandika Charles William.Akizungumza bungeni leo asubuhi, Lema amesema Simbachawene alimtaka yeye na viongozi wengine wa Chadema wamfanyie vurugu mkurugenzi huyo kisha tukio hilo lioneshwe katika Runinga ili waziri aingilie kati mgogoro huo kwa madai, utakuwa umedhihirika. “Nilimwambia Waziri Simbachawene kuwa Arusha tuna tatizo kwenye halmashauri tunaomba msaada, akanishauri tukafanye fujo ili aone kwenye vyombo vya habari na apate nafasi ya kuingilia mgogoro huo kwasababu rais amewapa nguvu wakuu wa mikoa. “Akaniambia siwezi kuja kichwa kichwa nenda kafanye fujo, mfungieni mkurugenzi nje halafu mimi nione kwenye TV ili niingilie mgogoro huo. Yaani waziri anaogopa kuingilia migogoro ...

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA TUKIO LA MOTO, BANDARINI JIJINI DAR LEO

Image
Moto ukiendelea kuwaka katika Makontena yaliandaliwa na kujazwa matairi kwa lengo la kufanya mazoezi, ingawa mitaani tayari zilikwisha enea habari kuwa moto mkuwa umeteketeza makontena, Bandarini jijini Dar es salaam leo. Afisa mawasiliano mkuu wa Bandari, Peter Milanzi, akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo ulipotokea moto ambapo alisema kuwa moto huo, ni sehemu ya mazoezi ya wafanyakazi wa Bandari ili kupima uwezo wa wafanyakazi wa Jeshi la kuzima moto na vifaa wanavyotumia wakati wa ajali za moto.  Aidha Peter, aliwaondoa hofu wananchi kwa kusema kuwa Makontena hayo yaliandaliwa na kujazwa matairi na kuyachomwa moto kwa lengo la kufanya mazoezi, ingawa mitaani tayari zilikwisha enea habari kuwa moto mkuwa umeteketeza makontena.  Baadhi ya majeruhi