Je, WAJUA WANAUME HUPENDA KUOA MWANAMKE WA AINA HII
Habari za wiki hii mpenzi msomaji. Mimi namshukuru Mungu kwa kuweza kunikutanisha na nyinyi kupitia safu hii ambayo pamoja na mambo mengine nazungumzia juu ya mada mbalimbali ambazo zinagusa maisha yetu ya kila siku. Wiki hii nitazungumazia juu ya aina ya wanawake ambao wanaume wengi hupendelea kuoa. Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha. Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri. Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sif...