SOMA JINSI WANAWAKE WANAVYO-SHAMBULIWA NA U.T.I
U.T.I kirefu chake ni Urinary Tract Infection ni maambukizi ya bakteria mbalimbali wanaoshambulia mfumo wa mkojo, yaani kwenye figo (kidney), kibofu cha mkojo na mifereji inayotoa mkojo (urethra) Mifereji inayotoa mkojo kwenye figo (ureter) na mfereji unaotoa mkojo nje, mara nyingi bakteria hushambulia sehemu za chini za mfumo wa mkojo yaani urinary bladder na kitaalamu kuitwa bladder infection. Bakteria hao baada ya kumuingia binadamu hupona mara moja pindi mgonjwa anapoanza dozi lakini kama wadudu hawa hawatatibiwa vizuri wanaweza kupanda na kushambulia figo na mshipa unaounga sehemu hiyo uitwao renal pelvis na kuleta madhara makubwa, hivyo kusababisha ugonjwa wa figo. Kuna wadudu wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wa binadamu ambao kila binadamu anaishi nao, hawa husaidia kulinda mwili na kitaalamu hujulikana kama normal flora na huwa ni askari wa mwili. Vijidudu hivyo hushuka hadi kwenye mlango wa haja kubwa na ku...