CHADEMA Wacharuka Baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda Kumweka Ndani Mbunge wao Saidi Kubenea..Watoa Tamko
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari na njia zingine za upashanaji habari tangu jana kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Ndugu Saed Kubenea aliwekwa chini ya ulinzi na kuamriwa kwenda kituo cha polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye inadaiwa hakutaka mbunge huyo azungumze na wananchi ambao ni Wafanyakazi wa Kiwanda cha Tanzania Took Garment, waliokuwa wamemuita mbunge huyo kwa ajili ya kumweleza matatizo wanayokumbana nayo kazini hapo, ikiwa ni pamoja na ujira kidogo na mazingira magumu ya kazi. Aidha akitambua kuwa alichofanya matumizi mabaya ya dhamana ya uongozi, hivyo akakusudia kuficha umma usijue uovu huo, katika tukio hilo Makonda aliwaagiza polisi wakamate kamera za waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo wakitimiza wajibu wao wa kikazi na kitaaluma kwa jamii. Katika hatua ya sasa, tunaomba kusema ifuatavyo; 1. Tukitambua kuwa mamlaka ya DC kuamuru watu kukamatwa y...