Posts

Showing posts from August 14, 2015

TAZAMA PICHA ZA MAPOKEZI YA LOWASA MBEYA

Image
Kutoka mbeya  hizi ni picha za awali kabisa za mapokezi ya mgombea wa UKAWA Edward lowasa wakati anaenda kutafuta wadhamini,Tizama hii.Picha nyingine zitakujia Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Ukawa kwa tiketi ya Chadema Mhe.Edward Lowassa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Ukawa baada ya kutua Jijini Mbeya leo kwa lengo la kujitambulisha .. Wapenzi wa Ukawa Jijini Mbeya wakati wa shamrashamra za kumpokea Mgombea Urais wa Ukawa kupitia Chadema Mhe. Edward Lowassa ambaye ametua Jijini humo leo.  Mgombea Urais wa UKAWA Kupitia CHADEMA Leo atakuwa Jijini Mbeya kwa ajili ya kutambulishwa na kusaka wadhamini. Hapa kuna picha kadhaa za shamrashamra za wananchi wakimsubiri kwa hamu kubwa uwanja wa ndege wa Songwe.

TCRA YATOA ADHABU KALI KWA TELEVISION YA ITV KWA HABARI ZA UONGO

Image
1.0 Utangulizi: Mnamo tarehe 10/08/2015, kituo cha ITV kilikiuka Kanuni za Huduma ya Utangazaji (Maudhui), 2005 kupitia kipindi cha Habari Zilizotufikia Hivi Punde kilichorushwa hewani kati ya saa 2.30 asubuhi hadi saa 5.30 asubuhi. Kipindi hiki kilikiuka Kanuni za Utangazaji kwa kutoa taarifa zisizo za kweli na za kichochezi zilizotangaza kwamba Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya mgombea wa CHADEMA Mheshimiwa Edward Lowassa. Taarifa hiyo ilikuwa na maandishi yaliyosomeka kama ifuatavyo:- 1. “ Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lapiga marufuku maandamano ya kumsindikiza kuchukua fomu mgombea Urais kupitia CHADEMA”. 2. “ Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lakanusha kupiga marufuku maandamano kutokea ofisi za CUF kuchukua fomu Mgombea Urais kupitia CHADEMA. Katika kuhitimisha taarifa hiyo mtangazaji alisikika akisisitiza kwamba Kamishina Suleiman Kova alisema ni marufuku maan...

RAIS KIKWETE AMZIKA KISUMO MWANGA

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la Kada Mkongwe wa CCM  Marehemu Mzee Peter Kisumo wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika huko kijijini kwake Usangi- Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mama Hosiana Kisumo Mke wa Marehemu Peter Kisumo wakati wa mazishi yake huko Usangi Mwanga Mkoani Kilimanjaro. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la Kada Mkongwe wa CCM Marehemu Peter Kisumo wakati wa mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Usangi- Mwanga Mkoani Kilimanjaro. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kilichowekwa kanisani wakati wa mazishi ya kada mkongwe wa CCM Mzee Peter Kisumo yaliyofanyika kijijini kwake Usangi-Mwanga Mkoani Kilimnjaro. (Picha na Freddy Maro)

ALICHOKISEMA PROF LIPUMBA BAADA YA KUREJEA NCHINI

Image
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alirejea nchini jana jioni akitokea Kigali, Rwanda alikokwenda mara tu baada ya kujiuzulu wadhifa huo siku nane zilizopita. Profesa Lipumba aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) saa 10.10 jioni kwa ndege ya Rwanda Air. Akihojiwa na Azam Tv kwa simu akiwa Kigali, siku tatu baada ya kuondoka nchini, Profesa Lipumba alisema alikuwa nchini humo akifanya utafiti kuona namna gani Tanzania inaweza kujifunza mambo ya kiuchumi kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika sekta hiyo. Alipoulizwa jana, Profesa Lipumba alisema akiwa huko alikuwa na mazungumzo na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB), wadau wa masuala ya rushwa, waziri wa fedha wa nchi hiyo na makamu mwenyekiti wa Bodi ya Utawala. “Wenzetu wamepiga hatua kubwa katika kukuza uchumi ndani ya kipindi kifupi, hivyo safari yangu ilikuwa ya kujifunza mbinu walizotumia kufikia malengo yao,” alisema....

ANGALIA PICHA LOWASSA ALIVYOWASILI MBEYA MUDA HUU

Image
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Ukawa kwa tiketi ya Chadema Mhe.Edward Lowassa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Ukawa baada ya kutua Jijini Mbeya leo kwa lengo la kujitambulisha .. Wapenzi wa Ukawa Jijini Mbeya wakati wa shamrashamra za kumpokea Mgombea Urais wa Ukawa kupitia Chadema Mhe. Edward Lowassa ambaye ametua Jijini humo leo.    CHANZO:  http://www.ajiratz.info/2015/08/angalia-picha-lowassa-alivyowasili.html

MAJINA YA WALIOTEULIWA UBUNGE, UWAKILISHI NA VITI MAALUM CCM YATANGAZWA RASMI

Image
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akionyesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya 2015-2020 ya CCM wakati wa kufunga kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mara baada ya kumaliza zoezi la kupitisha majina ya wagombea Ubunge na Uwakilishi mjini Dodoma.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipitia orodha ya majina ya waliopendekezwa kwenye nafasi za Ubunge na Uwakilishi,kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda. MNEC wa Wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete akipitia kitabu cha ilani ya Uchaguzi ya CCM kitakachotumika kwa mwaka 2015-2020.  Dk. Salim Ahmed Salim akipitia majina ya walioteuliwa wakatia wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mjini...