HUYU NI BINADAMU ALIYETAJIRIKA KUFUATIA KUJIBADILISHA MWILI WAKE NA KUWA KAMA MJUSI HUKO KWA WENZETU.
Jina alilopewa na wazazi wake ni Erik Sprague, ing awa Ulimwengu unamfaham kama Lizardman, huku akiwa na vipindi zaidi vya Television kibao akionesha jinsi alivyoweza kuubadilisha mwili wake huo. Mabadiliko hayo yanajumuisha kuchonga meno na kuwa makali, Tattoo mwili mzima ikiwa ya rangi ya kijani na magamba, Ulimi kupasuliwa kati na kuwa pacha, Manundu maalumu usoni na hivi karibuni hadi midomo yake imekuwa ya kijani yote. Kumekuwa na Uvumi kwamba huenda nyota huyo wa moenesho ya vipindi mbali mbali vya kutisha angefanya mpango aoteshwe mkia, lakini mwenyewe amekanusha na kusema jambo hilo haliwezekani. Mbali na shows kibao amekuwa mwandishi mzuri wa jinsi ya kuubadilisha mwonekano mwa mwili kupitia Body Transformation E-Zine Lizard Skynyrd ndo jina la Bendi yake ambayo imekuwa ikizunguka sehemu tofauti tofauti duniani kwa matamasha mbali mbali. CHANZO http://www.folclassic.com ...