Posts

Showing posts from September 8, 2018

BAD NEWS: AJALI YA MAGARI MATANO MBEYA, WALIOFARIKI WAFIKA 15

Image
IDADI ya watu waliokufa katika Ajali ya lori iliyogonga Magari mengine manne kabla ya kupinduka na kuwaka moto kwenye mteremko mkali wa Iwalanje, eneo la Igawilo jijini Mbeya imefikia 15, baada ya majeruhi wengine wawili kufariki dunia wakati wakipewa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya. Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Dk. Petro Seme amesema kuwa majeruhi wengine 13 wanaendelea na matibabu hospitalini hapo na kati yao wawili hali zao ni mbaya. Ajali hiyo imetokea jana tarehe 07 Septemba, 2018 majira ya saa 10 jioni katika mteremko wa mlima wa Igawilo Jijini Mbeya baada ya Lori lililokuwa na shehena ya viazi, likitokea Tukuyu kwenda Mbeya Mjini kuyagonga magari matano likiwemo basi dogo lililokuwa na abiria.

Ugomvi wa DC na Mkuu wa Mkoa wamkera Rais Magufuli

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amekemea tabia ya wakuu wa wilaya na mikoa kugombana wakati wanapotumikia wananchi. Ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi wa wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kikazi, ambapo kuna mgogoro mkubwa kati ya DC wa wilaya Glorius Luoga na mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Daud Ngicho na mkuu wa mkoa huo Adam Malima. Rais Dkt. Magufuli ameonyesha kukerwa na misiguano ya viongozi wa mkoa wa Mara unaofanya hata miradi mbalimbali ya maendeleo kukwama kufuatia DC Luoga na RC Malima kutofautiana. “Kwanini mnagombana, wewe DC uko chini ya RC Malima, umheshimu na si kugombana kila wakati mpaka shughuli za maendeleo zinakwama,”amesema JPM Hivi karibuni  Rais pia alikemea mgogoro kati ya mkuu wa wilaya ya Chemba na Naibu waziri wa Fedha, Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wa wilaya hiyo wakati wa kuzindua barabara inayounganisha Afrika.

Chozi la Mkurugenzi wilaya ya Serengeti lamuokoa kutumbuliwa na Mh. rais

Image
Mkurugenzi wilaya ya Serengeti bwana Juma Hamsini ameepuka rungu la Mh. rais Magufuli la kutumbuliwa baada ya mbunge wa wilaya hiyo kupitia chama cha Chadema bwana Marwa Ryoba kumtaka Rais kuchukua uamuzi wa kumuondoa mkurugenzi huyo. Bwana Marwa amedai kuwa mkurugenzi huyo ni mwizi sana ndio tatizo la wilaya hiyo kutoendelea mbunge huyo alisema:-“Mimi nakupenda Mh rais lakini kwa mkurugenzi huyu tuna mkurugenzi mwizi, naomba niseme ameenda WMA akawalaghai wakampa milioni ishirini akaenda akakutana na aliyekuwa rasi wa mkoa akampa rasi wa mkoa milioni tatu akarudi milioni kumi na sana akaweka mfukoni eti anaenda kumugawia mkuu wa wilaya hakuwagawia akaweka mfukoni mpaka leo,Takukuru mkoa wanajua wilaya wanajua” mbunge huyo aliongeza ” Mh. rais sio hilo tu juzi kwenye kamati ya bunge mkurugenzi huyu wamefukuzwa na kamati ya bunge kutokana na fedha za miradi ya maendelea ambazo hazionekani kwa mujibu wa taarifa za CAG kwenye vikao pia haji,kwahiyo mh;rais mimi sio kw...

Mwanakwaya Aliyeuawa Gesti, Familia Yasimulia Mazito

Image
D AR ES SALAAM: Tukio la mwanakwaya wa Kwaya ya Vijana ya Kanisa la AICT-Chang’ombe (CVC) Mariam Charles, 25, (pichani) mkazi wa Keko Furniture, wilayani Temeke jijini Dar aliyekutwa ameuawa kwenye Gesti ya East London, Mtaa wa Kwa Hamad Bonge, Temeke limeendelea kutikisa mjini na Risasi Jumamosi linakupa undani wake. Tukio hilo linadaiwa kutokea Septemba 5, mwaka huu katika nyumba ya wageni aliyokuwa amefikia mchumba wake aliyetajwa kwa jina la Frank ambaye amehusishwa na mauaji hayo. TUMSIKILIZE KAKA WA MAREHEMU Akizungumza  kaka wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Enock Charles, alisema kwamba alipata taarifa za kifo cha mdogo wake siku ya Jumatano (Septemba 5) asubuhi baada ya kutumiwa ujumbe na mama yao mzazi. “Mimi ninaishi Kigamboni, Jumatano asubuhi nikiwa kwenye mishemishe zangu, mama alinitumia SMS kwamba kuna matatizo nyumbani. “Nilimuuliza ni kuhusu nini akaniambia ni kumhusu Mariam. Nilishangaa kwa maana siku ya Ijumaa (jana) tulikuw...