Zari Amlilia Masogange, Akumbuka SMS Zake
Video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’ enzi za uhai wake. MPENZI wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’, kupitia akaunti yake ya Snapchat. Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Zari ameeleza kuwa Masogange alikuwa akimtafuta kupitia simu kila mwezi akimuulizia maendeleo ya watoto wake ingawa hawakuwa marafiki sana. Kupitia Mtandao wa Snapchat Zari ameandika; We were not friends as such but ever since you got my number you’ve been dropping me a text every month and i mean no month passed without you asking how are the kids. in peace sis.