Posts

Showing posts from March 8, 2017

VANESSA MDEE MIKONONI MWA POLISI

Image
Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limemshikilia Mwanamziki Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya. Mwanasheria wake, Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja majina ya wanaojihusisha biashara hiyo pamoja na watumiaji mapema mwezi uliopita. Mwanasheria Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa. Pia aliongeza kuwa Polisi walikwenda Nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi. Vanessa Mdee ni Mtanzania wa kwanza kuwa mtangazaji wa MTV VJ, Mdee, alizaliwa mwaka 1988 Arusha, alianza kufahamika zaidi mara baada ya kutangaza kwenye Redio na Luninga kwenye vipindi kama Epic Bongo Star Search na Dume Challenge na baadae kidogo wakati ananza kujikita kwenye muziki alikuwa ch...

VIROBA VYA BILIONI 5 VYAKAMATWA DAR

Image
KATONI 32,634 za pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 5.18 zimekamatwa jana, katika operesheni maalumu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uingizaji, uuzaji na matumizi ya pombe hizo. Pombe hizo zimekamatwa katika operesheni inayoendelea katika mikoa mitatu ya Kikodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dar es Salaam ambayo ni Temeke, Kinondoni na Ilala. Akizungumza katika operesheni hiyo, Mkaguzi kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), John Nzila alisema walikamata katoni 14,393 za konyagi, katoni 9,964 za Vradmill, Zanzi 31 na Valeur. 268. Alisema mzigo huo ulikutwa katika ghala la Loverira Enterprises lililopo Kimara Temboni na kwamba mzigo huo umezuiwa kwa hatua zaidi. Kwa upande wake Mwanasheria Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Heche Suguta alisema kuwa walikamata katoni 7,000 ...

MTANGAZAJI DJ FETTY KUREJEA CLOUDS FM LEO

Image
Dunia inaadhimisha mchango na thamani ya Wanawake duniani kila inapofika Tarehe 8 March kila mwaka.Kila nchi inakuwa na utaratibu wake wa namna gani wa kusherehekea ama kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.Wapo Wanawake wengi ambao wameleta alama chanya ya mabadiliko kwenye tasnia mbalimbali ikiwepo tasnia ya Burudani.Huwezi kuwataja kwa majina Wanawake wote ila wapo wengi ambao walileta mabadiliko yakaonekana kwa kile walichokuwa wanafanya. Clouds Fm kulikuwa na sauti moja nzuri hivi katika Dakika 180 katikati ya wanaume wawili wakorofi in town.Ushajua namzungumzia nani eeeh! Basi vunga Kama umeshamfahamu niwatonye washkaji ambao hawakubahatika kumsikiliza sauti yake.Binti wa kisukuma Fatma Hassan muite Dj Kwefeee ukipenda Fetty siku ya kesho anadondoka mjengoni kuiongoza show namba moja ya kijanja Xxl kuadhimisha siku ya Wanawake duniani.Dj Fetty ambaye aliondoka Clouds mwaka 2015 baada ya kuomba kupumzika aendelee na mishemishe zake siku ya kesho atakuwepo mje...