Posts

Showing posts from May 13, 2017

Ebola yauwa watatu Congo

Image
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kwamba ugonjwa wa Ebola umezuka katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Msemaji wa WHO nchini humo Eugene Kabambie amesema shirika hilo limechukua hatua hiyo baada ya watu watatu kufariki wakishukiwa kuwa na Ebola eneo hilo tangu Aprili 22. WHO imesema mlipuko huo unaathiri maeneo ya msituni ya Aketi, katika mkoa wa Bas-Uele karibu na mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Waziri huyo alikuwa ameiandikia WHO barua akiomba usaidizi katika kudhibiti ugonjwa huo. Shirika hilo limesema Waziri wa Afya wa DR Congo Oly Kalenga kupitia barua, alisema kulikuwa na watu tisa kutoka eneo la kiafya la Likati na Aketi waliohofiwa kuwa na Ebola. Watano kati yao walipimwa na mmoja wao akathibitishwa kuwa na virusi hivyo. Watatu kati ya tisa hao walifariki. "Ni kisa kilichotokea eneo lililo mbali sana, lenye msitu mkubwa, kwa hivyo tulikuwa na bahati kiasi.

Pogba apata pigo , afiwa na Baba ake mzazi

Image
Baba mzazi wa kiungo wa Manchester United, Paul Pogba, Fassou amefariki dunia jana usiku akiwa na umri wa miaka 79. Fassou Antoine Pogba alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu kabla ya kukumbwa na mauti hayo familia ya Pogba imethibisha kutokea kifo hicho katiak hospitali ya Le Parisien. Fassou mwenye asili ya Guinea alihamia Paris, Ufaransa miaka 30 iliyopita nchi ambayo Paul anaichezea katika mashindano ya kimataifa. Watoto wake wengine ni mapacha Florentin na Mathias wenyewe wameamua kucheza nchi anayotokea baba yao Fassou. Fassou alipiga picha akiwa jukwaani wakati wa fainali ya Euro 2016 zilizofanyika Ufaransa, akiwa na Florentin na Mathias  washangilia Paul akichezea Ufaransa dhidi ya  Uswisi. Mwezi Machi, kiungo wa Manchester United, Paul alituma picha katika Instagram akisherekea sherehe ya baba yake kutimiza miaka 79.

Picha: Treni ya Abiria Yapata Ajali, Morogoro

Image
MOROGORO: Treni ya abiria iliyokuwa inakwenda Bara imepata ajali usiku wa kumakia leo majira ya saa 5:25 katika eneo la Stesheni ya Mazimbu mkoani Morogoro. Katika ajali hiyo ilihusisha mabehewa saba ambapo manne yakiwa yameegama na matatu yameacha reli. Abiria mmoja, Ashura Mrisho aliyekuwa anasafiri kwenda Tabora amepata maumivu baada ya kuangukiwa na mizigo iliyokuwamo ndani ya moja ya mabehewa hayo. Mabehewa 13 yamerejeshwa Morogoro kuwapangia usafiri mbadala abiria waliokuwa wakisafiri na treni hiyo. Aidha Shirika la Reli Tanzania (TRL) linafanya utaratibu wa kuwasafirisha abiria wa bara kwa mabasi hadi Kijiji cha Lukobe Manispaa ya Morogoro ambapo watapanda treni kwenda bara. Kuhusu wale wa treni ya kuja Dar es Salaam kutoka bara ambayo itasimama Lukobe, watasafirishwa kwa mabasi kurudi Morogoro kuendelea na safari. Taarifa zaidi zitafuata wakati uongozi wa TRL, mafundi na wahandisi wakishughulikia ajali hiyo.

Ajali ya Basi na Lori la Mizigo Yaua Watu 19, Nakuru

Image
NAKURU, KENYA: Watu 19 wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya basi kugongana uso kwa uso na lori nchini Kenya. Ajali hiyo imetokea eneo la Mbaruk Jumamosi katika barabara kuu ya Nakuru-Nairobi, Mkuu wa polisi Nakuru, Hassan Barua amesema. Basi hilo ambalo ni mali ya kampuni ya Highway Sacco lilikuwa linaelekea Busia likitokea Nairobi wakati ajali hiyo inatokea. Kamanda Barua amesema dereva wa basi hilo alikuwa anajaribu kulipita lori ndipo alipogonga gari la mzigo lilokuwa linakuja mbele yake. Dereva huyo alikimbia baada ya kutokea ajali hiyo, wamesema polisi. Watu kumi na nne wamelazwa hospitali ya St Mary Nakuru, Shadrack Musau ambaye ni muuguzi wa zamu amesema.

CCM yakana muuliko wa Chadema

Image
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekana kuwa na mwaliko wa kuhudhuria kongamano la kujadili dhana ya demokrasia na vyama vya upinzani litakalofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Ilala, linatarajia kuwashirikisha watu mbalimbali maarufu wakiwamo wanasiasa na viongozi wakuu wa vyama vya siasa. Mratibu wa kongamano hilo, Makongoro Mahanga alisema jana kuwa wamemwalika Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole ambao chama chao kimekana kupokea mwaliko huo. Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula alisema hakuwa na taarifa za kongamano hilo na kwamba yupo mkoani Dodoma kwa sasa. ‘Nani anaongoza hilo kongamano? Mbona mimi sina taarifa. Linahusu nini ?” alihoji Mangula. Hata Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Rodrick Mpogolo alipoulizwa alisema hana taarifa kama viongozi wa chama hicho wamealikwa kwa sababu naye yuko safarini

TRA yachunguza mapato ya Diamond

Image
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetanabaisha kuwa wameanza kufuatilia vyanzo vya mampoto vya Msanii nyota wa Muziki wa Bongo Flavar Nasib Abduli ( Diamond Platnum) ili  kumpangia kodi Srtahiki nayapaswa kulipa. Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo, amesema kuwa  TRA inazungumza na Diamond kuhusu nyanzo vyake vya mapato . “Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo''.amesema Kayombo.

Wenye Vyeti FEKI Kulipwa Mafao Yao

Image
Watumishi waliobainika na vyeti feki, watalazimika kusubiri mafao yao hadi utaratibu wa kuwalipa utakapofanyika. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Amina Mollel. Amina alitaka kujua ni hatua gani zitachukuliwa ili kuwalipa mafao yao wafanyakazi waliobainika na vyeti feki. Waziri Kairuki alisema, ofisi yake itaandaa utaratibu wa mafao ya wafanyakazi hao na pindi utakapokamilika, watajulishwa na kulipwa haki zao. Aidha,  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu, Anthony Mavunde, alisema kwamba seeikali inaendelea na mchakato wa kuunganisha mifuko ya jamii. Mavunde alisema hayo alipojibu swali la msingi la Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Almas Maige, aliyetaka kujua mchakato wa kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii, umefikia hatua gani.

Majani ya mpapai husaidia kutibu magonjwa yafuatayo.

Image
Habari yako mpenzi msomaji wa phars blogspot, ni matumaini yetu u mzima wa Afya tele na unaendelea na pilikapilika za hapa na pale katika kuyasaka mafanikio.  Lakini huwezi kuyapa mafanikio kama hatakuwa umeimarika kifya.  Hivyo kwa kuzingatia hayo tumeona ni vyema tukuletee makala hii ambayo itakusaidia katika kuimarika kiafya. Umuhimu wa majani ya papai katika kutibu magonjwa yafutayo: Majani ya papai husaidia kwa kiwango cha juu katika kutibu majeraha ya vidonda. Unachotakiwa kufanya ni. Chukua majani ya papai kisha yatwange twage mpaka uhakikishe yamesagika kabisa.  Kisha yapake majani hayo katika kidondo kisha yaache kwa muda wa saa moja hadi uhakikishe yale maji maji ya kwenye majani yameingia katika kidonda. Kumbuka: kuweka kidonda hicho katika hali ya usafi kila wakati ili kuzuia bakteria kuingia katika kidondo. Majani ya mpapai husaidia kutibu shinikizo la damu ( blood pressure). Unachokiwa kufanya ni Chemsha maji ya mot

BIBI HARUSI APEWA TALAKA SAA CHACHE BAADA YA NDOA

Image
Matumizi ya simu za mkononi hupelekea mtu unayekuwa karibu naye kimwili kuwa mbali nawe kiakili na mawazo ambayo ameyaelekeza kwa mtu anayewasiliana naye muda huo. Balaa zaidi ni ‘kuchat’ ambapo mtumiaji wa simu hupelekea hisia zake zote kwenye vidole vinavyoandika huku akimuacha aliyenaye akiwa mpweke.Hii imemgharimu bibi harusi aliyekesha akipokea salamu za pongezi kwenye simu na kumsahau mumewe. Fuatilia kisa hiki…! Mwanaume mmoja ameamua kumtalakisha mkewe saa chache baada ya kufunga ndoa, kwasababu mkewe huyo mpya alitumia usiku wao wote wa ‘fungate’ kuchat na rafiki zake. Kwa mujibu wa gazeti la Al Watan la Saudi Arabia, bibi harusi huyo alikuwa busy akipokea salamu za pongezi kutoka kwa rafiki yake akimsahau mumewe aliyenaye chumbani muda huo.“Bwana harusi alijaribu kusogea karibu naye na kimahusiano, lakini alishitushwa kuona mkewe anampotezea, hajibu anachoulizwa au hata kuonesha vitendo,” ndugu wa Bwana harusi aliiambia Al Watan. “Mwanaume alipomuu

Huu ndio Ukweli kuhusu ndege iliyovutwa kwa trekta

Image
NI kioja. Tangu lini ndege ndogo inayoonekana kuwa ya kubeba abiria ikatembea kwenye barabara za magari mitaani kwa kukokotwa na trekta? Hivyo ndivyo wananchi wengi wa maeneo ya Dodoma mjini, hasa kutoka Uwanja wa Ndege hadi Area C, ambako walikuwa wakijiuliza kutokana na kujiri kwa tukio hilo la aina yake. Na ndivyo ilivyokuwa pia katika maeneo mengine nchini, hususan kwa wale waliobahatika kuiona picha iliyosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii juzi, ikionyesha ndege ndogo yenye mwonekano wa kuvutia pichani ikiburutwa na trekta barabarani. Ni tukio lililotokea kutoka Airport kwenda Area D, kupitia barabara ya Maili Mbili, ambako ndege hiyo ilikuwa ikikatiza polepole kwa kukokotwa na trekta kiasi cha kuwashangaza mamia ya watu waliobahatika kushuhudia jambo hilo ‘live’. Kwingineko nchini, uvumi mwingi ukasambaa, ukiwamo ule uliokanushwa na Jeshi la Polisi kwamba ndege hiyo ilikuwa ikikokotwa baada ya kuanguka. Kutokana na yote hayo, ambayo mwishowe y

SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA UGENI KUTOKA BENKI YA NBC

Image
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Benki ya NBC ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Ndg. Nehemia Mchechu (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Bodi, Dkt. Kassim Hussein (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ndg. Edward Marks (kulia) uliotembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (Kushoto)akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya NBC, Ndg. Nehemia Mchechu (wa pili kushoto) akizungumza katika ugeni kutoka Benki ya NBC uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, anaefuata ni Mkurugenzi wa Bodi, Dkt. Kassim Hussein (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ndg. Edward Marks (kulia). (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Tatizo la Kunuka Kikwapa, tiba hii hapa

Image
Kikwapa  ni  tatizo la kutoa harufu mbaya  sehemu ya kwapani katika mwili wa binadamu. Tatizo la kikwapa husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu  chini ya kwapa. Tatizo la Kikwapa ni kero kwa sababu husababisha mtu kutoa harufu inayokuwa kero kwako na kwa mtu mwingine aliyeko jirani yako. Ili kwapa lako liwe na harufu nzuri, kavu na safi fanya yafuatayo Paka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa  safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya Oga kila siku na safisha nguo kwa maji safi itasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa. Osha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated soaps) Punguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vi

KIJANA ALIYEMUUA MPENZI WAKE NA KUMCHOMA MOTO AKAMATWA SOUTH AFRIKA

Image
Polisi wa nchini Afrika ya kusini wamethibitisha kumshikilia kijana wa miaka 27 na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya mpenzi wake Karabo Mokoena mwenye umri wa miaka 22 aliyeripotiwa kupotea wiki mbili zilizopita. Mwili wa binti huyo ulikuwa ukiwa umechomwa na ilikuwa vigumu kuutambua. Wanawake wengi wa nchini humo kupitia mitandao ya kijamii walionyesha kukasirishwa na kitendo hicho na kulaumu vitendo vya uonevu dhidi ya wanawake. Nchi ya Afrika Kusini imeripotiwa kuwa na matukio mengi ya udhalilishaji na vitendo vya uonevu kwa wanawake ikiwamo ubakaji kwa muda mrefu sasa. Huyu Ndio Kijana Aliyemuaa Mpenzi wake

Shamsa Adaiwa Kumfirisi Mumewe, ni baada ya mambo kubadilika

Image
DAR ES SALAAM: Ikiwa ni miezi nane tu imepita tangu aingie kwenye ndoa, staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford anadaiwa kumfilisi mumewe, Rashid Said ‘Chid Mapenzi’, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili. Chanzo makini ambacho ni ndugu wa mume wa Shamsa kililiambia Risasi Jumamosi kuwa mwanamama huyo tangu aolewe, maisha ya Chid Mapenzi yamebadilika kwani hata biashara zake haziendi vizuri jambo ambalo linaonekana kuwa mwanamke huyo amempa gundu. “Kiukweli Shamsa ni kama amempa gundu mumewe kwani tangu waoane mambo siyo mazuri, amekuwa akimkataza kuwa hata na marafiki zake jambo linalowachukiza sana ndugu maana anamrudisha nyuma ndugu yao. “Angalia mpaka duka walilokuwa nalo pale Mwananyamala-Komakoma wamelifunga na vitu vimerudishwa nyumbani hivyo wanauzia nguo na viatu nyumbani. “Kilichosababisha wakafunga pale ni kwamba kwanza Shamsa anaringa sana pia kodi iliwashinda kwani walitaka kutoa ya miezi mitatu baada ya kodi waliyolipia kuisha hivyo mwenye nyumb

Jambazi Sugu Mwanamke Auawa

Image
NAIROBI: Mwanamke anayedaiwa kuwa jambazi sugu, Claire Mwaniki ambaye amekuwa akipakia mtandaoni picha zake akiwa amejipodoa na kujipamba, ameuawa na polisi katika Mtaa wa Kayole jijini Nairobi, Jumatano alfajiri. Gazeti la Daily Nation limeeleza mwanamke huyo alikuwa na majambazi wengine wanne wa kiume wakati walipofumaniwa na polisi wakitekeleza tukio la kupora kwa kutumia sialaha (ujambazi) katika eneo la Lower Chokaa, Mtaa wa Kayole. Mwanamke huyo anadaiwa kuwafyatulia risasi maofisa wa polisi akiwa na jambazi mwingine lakini polisi walipambana nao hadi kuwaua majambazi wawili akiwemo Claire Mwaniki huku wenzao wakifanikiwa kutoroka. Taarifa za Gazeti la Daily Nation inasema polisi waliwaandama baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wenzao kupitia mtandao wa WhatsApp kwamba majambazi hao walikuwa wamekwepa mtego waliokuwa wamewekewa ambapo polisi walijiandaa na kisha wakawakabili katika Mtaa wa Lower Chokaa. Mkuu wa Polisi wa Mtaa wa Kayole, Joseph Gichangi

BALOZI DK.MAHIGA AKABIDHIWA MAGARI NA SERIKALI YA KUWAIT

Image
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dk. Augustine Mahiga amepewa msaada wa magari kutoka serikali ya Kuwait ilikuweza kusaidia katika shughuli mbalimbali za kiutendaji.Balozi Mahiga amesema hayo wakati akipokea msaada wa magari kwa ajili ya wizara yake amesema wizara yake sio yenye tatizo ya usafiri bali ni suala wizara mbalimbali na taasisi zingine za serikali .Amesema serikali ya Kuwait inatoa msaada katika serikali ya Tanzania zaidi ya dola za kimarekani milioni 200 kwa kila mwaka.Balozi Mahiga amesema ubalozi wa Kuwait nchini amekubali kusaidia magari kwa sekta zingeni kwa kutaka kuorodhesha mahitaji ya usafiri ili kuweza kusaidia serikali ya Tanzania Kiutendaji. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukabidhiwa magari kutoka ubalozi wa Kuwait nchini leo Jijini Dar es Salaam. Balozi wa Kuw

Job Posts at Moshi Urban Water Supply and Sanitation Authority [MUWSA]

Image
Moshi Urban Water Supply and Sanitation Authority [MUWSA] is a full autonomous utility responsible for the provision of safe water and collection and disposal of wastewater in Moshi, the town of Mt. Kilimanjaro. MUWSA is looking for dynamic, results driven individual to fill in the position of Finance Manager 1.0 Purpose of the Job This is a managerial position in which the position holder will be responsible with the entire management of Authority's financial assets as per the required national and international standards. 2.0 Main duties and responsibilities: i. The Finance Manager is the head of Department responsible for finance and supplies. ii. Controls financial and supplies affairs of the Authority. iii. Ensures that the Authority's financial assets are properly safeguarded and maintained. iv. Establishes, administers and co-ordinates the funding requirements of the' Authority. v. Provides financial advice to the Managing Director and the Bo

Job Post at World Health Organization Tanzania , May 2017

Image
NPO - Hiv/Aids - (1700996) OBJECTIVES OF THE PROGRAMME The objectives of the WHO Regional Office and the CDS Cluster are to assist Member States to rapidly scale up access to treatment and care whilst accelerating prevention and strengthening health systems to make the health sector response to HIV/AIDS more effective and comprehensive. This includes the provision of intensified technical and resource mobilization support to Member States in an effective, appropriate and timely manner, by increasing WHO technical assistance and resources at country level to assist the government and other key partners in developing and implementing a national scale-up plan for HIV/AIDS prevention, care, treatment and support. DESCRIPTION OF DUTIES Under the direct supervision of the WHO Representative, the incumbent's duties shall be to:1) Support the Ministries of Health (Mainland & Zanzibar) in developing strategies for increased and equitable access to HIV prevent