Posts

Showing posts from February 20, 2015

Aunt Ezekiel Aporomosha Maneno Machafu, Kisa Picha Akiwa Kiwanja Anakula Bata!!

Image
Mrembo na mwigizaji wa filamu za kibongo, Aunt ezekiel amejikuta akitoa maneno makali baada ya mashabiki wake kumshabulia kwa maneno baada ya kuweka mtandaoni picha ikimuonyesha amevalia kinguo ambacho kwa maoni ya mashabiki hao hakistahili kuvaliwa na mwanamke mjamzito na kibaya zaidi alionekana mkononi ameshika shupa ambao wengi waliiona kama niyakilevi. Aunty Ezekiel alibandika picha hiyo hapo juu hivi juzi kati akiwa na jamaa kwenye ukurasa wake mtandaoni na kuandika maneno  “My best friend,my love,my kimoko I love him so much” Baada ya kubandika ujumbe huo baadhi ya mashabiki wake walionyeshwa kukera na mavazi na sehemu alikokuwepo nalumtaka atulie nyumbani alee mimba yake kwani kwasasa inaonekana kuwa na ya zaidi ya miezi nane na wiki kadhaa. “Ungetulia  tu nyumbani ukasubirikujifungua salamamjamzito kuzurura namna hiyo na mijanaume sio poakabisa tena na kilaji mkononi harafu pia hata hayo mavazi mmmh!! ” alisema mmoja wa shabiki na kuungwa mk...

WHEN WEMA DOING THIS WITH PETIT MAN, DIAMOND DID THIS WITH HIS 41YRS GIRLFRIEND ZARI.

Image

KIKONGWE ALIYEPIGWA MAWE KWA MADAI YA USHIRIKINA HALI MBAYA

Image
Kikongwe akiwa hoi baada ya kupigwa mawe kutokana na imani za kishirikina.Kikongwe huyo na Maurus Zenda (46) anayedaiwa kuwa ni mwanaye kiukoo, kwa pamoja walijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na baadhi ya ndugu zake kwa kuhisiwa kuhusika katika upotevu wa mtoto Adamu Mselewa (4). Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia wa ukoo huo, hali ya bibi huyo bado ni mbaya na wanajitahidi kwa hali na mali kuokoa maisha yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alikolazwa. “Bado hali ni mbaya, bibi bado analalamika maumivu, tunaendelea na matibabu huku tukisubiri madaktari watatueleza nini kuhusu maendeleo yake, ikishindikana hapa tutamhamisha hospitali, afadhali kidogo Maurus,” alisema mwanafamilia huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake. Mtoto wa kikongwe huyo.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Mihayo Msekhela, waliwakamata watuhumiwa 10 kutokana na tukio hilo, ambao ni Ambros Mselewa (24) ambaye ni baba mzazi wa mtoto aliyepotea, Maria Zenda (45), Lamec...

Uteuzi wa Paul Makonda Kuwa Mkuu wa Wilaya Wapingwa Kila Kona.....Anatuhumiwa Kumpiga Warioba na Kumtusi Lowassa Hadharani

Image
Uteuzi wa Makonda ambao umefanywa na Rais Kikwete, unaonesha kuwashitua wengi; hali ambayo imefanya watu wengi kumbeza hasa kupitia mitandao ya kijamii.   Baadhi ya wanaobeza, wanadai kwamba Makonda hana sifa ya kuongoza wilaya kubwa kama Kinondoni, ambayo ina changamoto na migogoro mingi ya ardhi.   Makonda ambaye ni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa UVCCM, jina lake limekuwa kubwa hivi karibuni baada ya kutuhumiwa kumpiga  Jaji Warioba wakati wa  mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere.   Pia, kujitokeza kwake hadharani kumpinga Edward Lowassa, kuliongeza jina hilo kuwa maarufu. Wakizungumza na Phars blog  kwa nyakati  tofauti, baadhi ya wasomaji wa mtandao huu, wamedai kuwa uteuzi huo wa Rais ni mzuri ila  alikosea kumweka wilaya ya  Kinondoni yenye matatizo chungu mzima ya kiutendaji ikiwemo migogoro ya mipaka, ardhi, wafanyabiashara ndogondogo na mambo mengine ya ndani. “Tunampongeza...

BREAKING NEWZ:Muimbaji wa Chamber Squad Mez B afariki dunia

Image
Muimbaji wa kundi la Chamber Squad, Maze B, amefariki leo saa nne asubuhi, kwa mujibu wa mtu aliyekuwa akimuuguza.    Msanii huyo aliyewahi kufanya vyema na wimbo wake ‘Fikiria’ alikuwa amelazwa katika  hospitali ya Mwananchi mjini Dodoma. Mez B aliyezaliwa kwa jina la Moses Bushagama alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Pneumonia.   Hivi karibuni aliongea na E-News ya EATV na alikuwa anaendelea vyema:   “Nilikuwa na tatizo la Pneumonia tokea mwezi wa 12 nikawa nipo vizuri nilivyo kuja tena Dodoma hali ikabadilika ndo nipo hospitali nimelazwa nasumbuliwa na maumivu ya kichwa na shingo,” alisema.   “Nategemea kuruhusiwa muda wowote na sasa hivi naendelea vizuri.”    Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

WAKALA WA KUTEKA ALBINO, AUAWA KWA MOTO

Image
Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika kijiji cha Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo. Wananchi wa vitongoji vya Kazunzu, kijiji cha Nyambemba, kata ya Kazunzu, wakishirikiana na wa kitongoji cha Lueseselo, kata ya Bulyaheke, wamempiga kwa marungu, mawe na mapanga na kisha kumchoma moto mtu ambaye bado hajafahamika, wakimtuhumu kuwa wakala wa kuteka watoto wakiwamo walemavu wa ngozi (albino), akishirikiana na waganga wa kienyeji wapiga ramli kwa imani za kishirikina za kupata utajiri. Mbali ya kumuua, wananchi hao pia wamevunja na kuchoma moto nyumba 13 zilizoezekwa kwa bati mali ya mganga wa kienyeji mwanamke mpiga ramli mwenye umri wa miaka 40 (jina linahifadhiwa). Hata hivyo, mganga huyo na familia yake walifanikiwa kuwatoroka wananchi hao. Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ...

Uteuzi wa Paul Makonda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni bado waendelea kupingwa na wengi

Image