Posts

Showing posts from November 17, 2015

RAIS MAGUFULI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KATIKA UBALOZI WA UFARANSA NCHINI

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.(Picha na Ikulu)   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak Tanzania mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ...

Chanzo Lulu Kutodumu na Wanaume Chatajwa

Image
 Ubuyu! Licha kujaliwa umbo matata na mvuto wa aina yake, staa wa Bongo Movies Elizabeth Michael ‘Lulu’, anadaiwa kutodumu na mwanaume, Ijumaa Wikienda limetajiwa chanzo cha hali hiyo. Kwa mujibu wa sosi wa ndani wa familia ya staa huyo, chanzo kikubwa cha Lulu kutodumu na mwanaume anayempata kama mwandani wake ni mama yake, Lucresia Karugila. Ilidaiwa kwamba, kama ilivyokuwa kwa Wema Sepetu zamani, mama yake, Miriam Sepetu alidaiwa kumwekea ‘patroo’ mrembo huyo kwa kumchagulia mwanaume wa kuwa naye, jambo lililomfanya Wema ashindwe kudumu na mwanaume mmoja. “Hiyo ndiyo hali halisi inayomkuta Lulu. Yaani ni kama Wema zamani,” kilisema chanzo hicho. “Unajua mama Lulu anataka mwanaye awe na mwanaume mwenye fedha ili amsaidie kuhudumia familia. “Inapotokea mwanaume anashindwa kuhimili matumizi, basi mama huyo humtaka mwanaye kusitisha uhusiano huo mara moja kwani unakuwa si wa masilahi,” kilidai chanzo hicho. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilitinga n...

BREAKING NEWZZ...ALIYEKUWA MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA KIGOMA KUSINI DAVID KAFULILA AIBUKIA MAHAKAMANI

Image
Hatimaye David Kafulila afungua Shauri Mahakama kuu kanda ya Tabora Lakupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Kigoma Kusini,Ameitaka Mahakama hiyo Kumtangaza Mshindi

HATIMAYE UKWELI KUHUSU CHUKI YA ZITTO KWA MSICHANA MSOMI DR. TULIA YATAJWA KUMBE KUNA MENGI NYUMA YA PAZIA

Image
Jamii ya wanazuoni imekuwa ikijiuliza ni kwanini mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe anampiga vita mgombea unaibu spika Dk.Tulia Ackson. Wanahoji ni kwanini Zitto Kabwe anamhofia huyu mwanamama wakati ana vigezo vyote vinavyompa "credibility" ya kugombea.Imefikia hatua Zitto anamnadi Mussa Azzan ambaye ni mbunge wa Ccm na kusahau kuwa yeye ni mpinzani ndani na nje ya bunge. Hapa ndipo dhana ya usaliti kwa Zitto Kabwe inapozidi kumea kwenye masikio ya watanzania.Zitto Kabwe hataki kukubali kuwa siasa ya bunge sio yake peke yake. Mnakumbuka sakata la aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TPDC ambaye PAC ikiongozwa na Zitto Kabwe iliamuru akamatwe na kuwasilishwa polisi!?Tena kwa makosa ambayo PAC ilikuja kuangukia pua!! Namzungumzia Andilile Mwainyekule.Huyu ni mume wa ndoa wa Dk.Tulia Ackson.Zitto Kabwe anauona ugumu wa yeye kuiyumbisha serikali kwa skendo za kupika kama kiti kitasimamiwa na Dk.Tulia Ackson. Zitto Kabwe anahofia Dk.Tulia Ackson kutumia mwanya wa...

MAMA: Miezi 11 Mwanangu Anaishi Kwa Mateso Bila Upasuaji!

Image
Mtoto Asmina Abdallah. Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa Mtoto Asmina Abdallah mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minne, mkazi wa Kijiji cha Mgambo, Unguja, Zanzibar anaishi kwa mateso bila kufanyiwa upasuaji kwa madai ya kutokamilika kwa vipimo kufuatia upungufu wa mashine katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto Asmina Abdallah akiwa na mama yake, Amina Maburuki Amani.Maisha ya mtoto huyo kwa sasa yapo hatarini kutokana na uvimbe uliopo machoni kuongezeka na haujapatiwa ufumbuzi wa matibabu kwa miezi 11 huku ukienda sambamba na maumivu makali.  Akizungumza na waandishi wa habari hii wiki iliyopita katika wodi ya watoto ya Makuti A Muhimbili, mama mzazi wa mtoto huyo, Amina Maburuki Amani alisema kwamba hali ya mtoto wake inazidi kuwa mbaya na anaelekea kukata tamaa.  Akifafanua zaidi mama huyo alikuwa na haya ya kusema:  “Hali ya mtoto wangu imekuwa ikibadilika kila kukicha huku akilia kutokana na maumivu makali, nimechoka safar...

KOBE 201 WALIOKUWA WAKISAFIRSHWA NJE YA NCHI WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA J.K NYERERE

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akikagua mabegi matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa kuamkia leo na askari wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.   Watuhumiwa hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi wa Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi lakini mbwa maalum (sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa pamoja watuhumiwa hao walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini Malaysia.  Kobe wapatao 201 waliokamatwa na askari wanyamapori kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mbwa maalum (sniffer dogs).      Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Dorina Makaya kulia na Mmoja wa Askari wanyamapori wakiangali...