Posts

Showing posts from June 27, 2013

FILAMU MPYA YA AUNT EZEKIEL YAZUILIWA BAADA YA KUWA NA VIPANDE VYENYE KUCHOCHEA NGONO

Image
SERIKALI kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji, Aunt Ezekiel na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya iitwayo Scola vinginevyo haitaruhusiwa kuingia mtaani. Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo inayosimamia maadili ya sinema za Kitanzania, imeeleza kuwa Aunt aliipeleka  filamu hiyo ili ikakaguliwe kama zilivyo taratibu lakini bahati mbaya ikagundulika kuna ‘sini’ tatu ambazo zilitoka nje ya maadili ya mtanzania. “Kuna vipande vitatu ambavyo kimsingi vimevuka matakwa ya maadili ya Kitanzania hivyo hakuna jinsi, lazima avitoe kama anataka kuiingiza sokoni sinema hiyo,” kilieleza chanzo makini ndani ya bodi hiyo kilichoomba hifadhi ya jina. Kabla ya mwandishi wetu hajazungumza na Aunt, alimpata rafiki wa karibu na staa huyo ambaye alifafanua kuwa rafiki yake (Aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo lakini bado yupo katika mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee.   “Amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie m

WATANZANIA WAISHIO MIKOANI WAPIGWA MARUFUKU KWENDA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA

Image
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo. Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake. Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.   “Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.   Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza

ULINZI WA RAIS OBAMA JIJINI DAR NI BALAA....MITAMBO MBALIMBALI YA MAWASILIANO IMEFUNGWA UWANJA WA NDEGE WA KIA

Image
Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini. Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea. Ulinzi haujawahi kutokea Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo. Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa. “Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege zitabadilika

WATANZANIA WAISHIO MIKOANI WAPIGWA MARUFUKU KWENDA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA

Image
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo. Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake. Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.   “Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.   Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanz

SHILOLE AMTIMUA MDOGO WAKE BAADA YA KUJAZWA MIMBA AKIWA MIKONONI MWAKE

Image
STAA wa sinema za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ (pichani) amemtimua mdogo wake aliyekuwa akiishi naye aitwaye Mary baada ya kunasa ujauzito.   Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kimepenyeza habari kuwa, Shilole alifikia maamuzi hayo baada ya kumuonya binti huyo aachane na mwanaume aliyemjaza mimba hiyo lakini hakusikia hivyo akaona bora amtimue.   “Kamtimua baada ya kumuonya mara nyingi bila mafanikio akaona isiwe tabu bora aepuke aibu,” kilisema chanzo hicho. Alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo, mdogo huyo wa Shilole alikiri kutimuliwa na sasa amehamishia makazi kwa jamaa yake anayefahamika kwa jina la Tonny Montensi anayeishi Sinza, jijini Dar.

MILIONI 15 ZAHITAJIKA KWA MGANGA WA KIENYEJI ILI KUMRUDISHA KATIKA HALI YA KAWAIDA BAADA YA MAITI KUFUFULIWA UKO MKURANGA PWANI

Image
BINTI aitwaye Nuru Omari anayedaiwa kufariki dunia mwaka 2010 ameibuliwa hivi karibuni wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani na mganga akiwa hai kwenye banda kuukuu. Binti Nuru Omari aliyeibuliwa. Tukio hilo limetokea kwenye Kijiji cha Kalole, Tarafa ya Kisiju, walayani humo. Kwa mujibu wa baba wa binti huyo, Omari Salum, mwaka 2010 ndugu wa mkewe aitwaye Nyasenene aliyekuwa akiishi Charambe Mbagala, jijini Dar alifika nyumbani kwake na kuwaomba wampe mtoto wao kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za ndani ‘hausigeli’. Kijumba alimokuwa Nuru. Baada ya binti huyo kufanya kazi kwa muda mfupi aliugua malaria, baba mtu akapewa taarifa  na kufika Dar kwa ajili ya kumuona mwanaye  aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar. Mzee huyo amesema alikwenda Muhimbili na kufanikiwa kuzungumza machache na mwanaye huyo ambapo alikuwa akilalamikia maumivu ya tumbo.   Ndugu na majirani waliofika kumtazama Nuru. Mzee huyo alisema ilibi