Posts

Showing posts from January 4, 2018

Breaking News: BOT yazifutia leseni Benki Tano

Image
 Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imezifutia  leseni ya kufanya biashara benki tano na kuziweka chini ya ufilisi. Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na BoT imezitaja benki hizo kuwa ni Covenant Bank For Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited, na Meru Community Bank Limited. BoT imeeleza kuwa imefanya hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 56(1)(g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2)(i), 11(3)(c) na (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuzifunga; kusitisha shughuli zake zote za kibenki; kufuta leseni zake za biashara ya kibenki; na kuziweka chini ya ufilisi. “Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu Na. 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006; Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya Bima ya Amana (The DEPOSIT INSURANCE BOARD) kuwa mfiiisi kuanzia tarehe 04 Januari 2018,” imeeleza taarifa hiyo.” ...

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI, WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UGANDA SAM KUTESA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. < Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ujumbe Maalum uliotoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni na kuwasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiufungua na kuusoma Ujumbe huo maalum uliotoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni na kuwasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kute...

NUNUA JIKO TUKUPELKEE HADI KWAKO BUREEE (DAR) NA ZAWADI YA MAFUTA BUREEEE

Image
Kwa Mara nyingine tena Bngo Deco Electronics, tunakuletea majiko makubwa ya kupikia kwa bei poa kabisa. Majiko haya yanadumu sana na yanakuja na warranty  ya mwaka mmoja, likisumbua tu tutakurekebishia. Nakwa kuthamini mchanngo wa Muungwana Blog kila mteja atakatoka katika Muungwana atapew dumu la mafuta ya alizeti BUREE na kama yupo Dar tutampelekea BUREE hadi kwake.   Kwa wateja wa mkoani gharama za kutuma jiko kwenda mkoani ni jukumu la mteja mwenyewe ila kama ni kumpelekea kwenye basi au lori la kuja mkoani basi tutatoa usairi BUREE hadi sehemu ya kutumia. Tupo Magomeni Mapipa mtaa wa Idrissa karibu kabisa na Butiama Restaurant.

NANDY ACHARUKA BAADA YA TAARIFA KUSAMBAA KUWA ANATOKA NA RUGE MUTAHABA.

Image
January 3, 2018 kumekuwepo na post kwenye mitandao ya kijamii kuhusu msanii Nandy kudaiwa kutoka kimapenzi na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, Nandy ameamua kuandika kwenye ukurasa wake wa Istagram kuhusu tuhuma hizo. Nandy Kupitia ukurasa wake wa Isntagram ameandika kuwa. “Mtu akifanya mziki wake kwa amani bila drama kuna watu wanakuwa hawatosheki kabisa. hivi mimi ni kichaa mpaka kujiachia kama uyo msambaza habari anavyo sambaza!” “Kwani suala la watu kusema na toka na boss wangu nalijua leo au nigeni kwangu sana mpaka nijiachie kwenda naye ma camp sijui ma club kama mnavosema???” – Nandy “Embu tuwe na utu please kwa hiyo me nimekuwa wakuja kiasi kwamba mshamba kiasi nikashindwa kujificha na mashungi juu basi kama ni hivyo  tumeshindwa kupishana kusafiri atangulie ndo nifuate,”– Nandy “Kwani sijui hata kama ingekuwa ni kwa nia nzuri  msingesema mnazani mambo ni marahisi kiasi hicho tupeane heshima kuna watu we...