NJIA KUMI KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE
Ni makala muhimu sana. Wastani wa maisha ya Mtanzania ( na Waafrika wengi) hata wale waliosoma au wanaojiweza kiuchumi ni miaka 40-50. Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai wetu ni afya, unene na kutojua kujiangalia vyema afya zetu. 1-ULAJI Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na namna unavyokila. · Unavyokula. -Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. Tumbo lina musuli zinazofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili. (PENDEKEZO la kwanza. Asubuhi, kuny...