Posts

Showing posts from December 13, 2016

Mwanzilishi wa JamiiForums, Maxence Melo Akamatwa na Polisi, Anyimwa Dhamana

Image
  DAR ES SALAAM: Mwanzilishi, Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa selo katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Police Central) leo Desemba 13, 2016. Polisi wameeleza muda huu kwamba leo atalala ndani (selo) hadi kesho atakapofikishwa mahakamani. Imeelezwa kuwa, kosa la kushikiliwa na Jeshi la Polisi ni kukataa kutoa taarifa binafsi zilizohitajika za wateja wa mtandao anaoumiliki wa JamiiForums. Maxence ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa, kufanya hivyo ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi. Maxence Melo amekamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya Polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari. CHANZO: JAMII FORUMS

MSANII CHUCHU HANS ASEMA HAYA BAADA YA KUSHINDA TUZO

Image
  Ushindi wa tuzo ya Muigizaji bora wa kike wa Tuzo za EATV 2016 kumemtoa machozi Chuchu Hansy na kumkumbusha mambo mengi aliyopitia kwenye maisha yake. Muigizaji huyo ambaye hakuwepo kwenye usiku huo wa tuzo na kuwakilishwa na meneja wake, ametoa ya moyoni kupitia Instagram kwa kusema ushindi huo umemfanya akumbuke maneno aliyokuwa akipewa na mama yake katika kipindi cha ukuaji wake. “Naamini kuna uwepo wangu kwa kila hatua tupigayo, ama hakika usitamalaki ya moyoni kwa kuyadhihaki ya machoni. Hii imenipa funzo zaidi ya lile alilonipa mama nikiwa na vunja ungo,” alisema Chuchu. “Mama aliniambia heshimu watu bila kuwa dhihaki kwa makundi,ama kuwa bagua kwa rika,” “Niwashukuru wote mlio nipigia kura amahakika mme tenda vema,likini mimi sio bora kuliko wenzangu ila nadhani kwa wino wakura zenu ulistahili niwe BEST ACTRESS, niwashukuru zaidi na zaidi, nikiandika maneno haya machozi yananitoka lakini hii yote ni heshima mlio nivika NENO LA KALE NI ASANTE,” alio...