Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’akifanya yake na mke wake Grace Mgonjo baada ya kufunga ndoa. BAADA ya Jumamosi iliyopita Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ kufunga ndoa na mchumba’ke wa kitambo, Grace Mgonjo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo Posta jijini Dar na sherehe kufanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, ameibuka na kufunguka suala la Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu kuikacha harusi yake. Staa wa Bongo, Wema Sepetu. Taarifa za awali kutoka kwa chanzo makini zilieleza kuwa, Profesa Jay na Wema ambaye alihamia Chadema miezi kadhaa iliyopita wana bifu kali japokuwa haijulikani chanzo ni nini, ndiyo maana mwanadada huyo hakuhudhuria kwenye harusi hiyo. “Unajua Wema na Jay hawana uhusiano mzuri tangu ahamie kwenye chama hicho yaani wana bifu ndiyo sababu hata Wema hakuhudhuria kwenye sherehe ya harusi ya Jay...