Posts

Showing posts from September 14, 2017

Majibu ya Ndugai kwa Lema kuhusu lissu

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amejibu tuhuma za mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, na kumtaka asipotoshe wananchi, bali apeleke malalamiko yake kwenye kamati. Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiendesha bunge, na kusema kwamba bunge lina utaratibu wake kwenye kila jambo linalohusika bungeni hapo. "Lema asipotoshe wananchi aende hadharani kwenye kamati kuzungumzia hayo, bunge haliwezi kusimama kwa shambulio la Lissu bali kanuni zinasema mbunge akifariki bunge linasimama kwa siku moja. Na iwapo Spika akiletewa jambo la maadili linapelekwa kamati ya maadili, suala la jinai linapelekwa polisi", amesema Spika Ndugai Pia Spika Ndugai amesema suala la Tundu Lissu kuchangiwa fedha za matibabu na wabunge wakati yeye alitibiwa nje ya nchi ni kwamba matibabu ya Tundu Lissu yameenda kinyume na utaratibu wa bunge. "Wabunge wanaopelekwa nje (India) wanapewa rufaa kutoka hospital ya Muhimbili lakini si kama alivyop

Breaking News: Mahakama ya Kisutu yamuachia huru Yusuph Manji

Image
KISUTU: Mahakama imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo ikionyesha kuwa hana nia ya kuendelea na kesi dhidi yake. Manji na watuhumiwa wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na plate number mbili za magari ya serikali. Watuhumiwa wengine walioachiwa huru kwenye kesi hiyo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

JESHI LA POLISI DODOMA LASIKITISHWA NA KITENDO CHA DEREVA WA TUNDU LISSU KUTOFIKA POLISI

Image
        Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto ameeleza kusikitishwa kwao na kitendo cha dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutokufika polisi na kutoa maelezo yake. Kamanda Muroto amesema hayo leo Jumatano wakati akijibu swali la upelelezi unaendeleaje kuhusu tukio hilo. Amesema upepelezi unaendelea kuhusu tukio la Lissu kupigwa risasi na watu mbalimbali wanaendelea kuhojiwa wakiwemo wamiliki nane wa gari aina ya Nissan ambazo zilikamatwa kuhusiana na shambulizi hilo. Wamiliki wa gari tumewahoji na tunapogundua hakuna muunganiko wowote basi tunaachana nao maana hakuna haja ya kuendelea kuwashikilia au kushikilia gari hizo,” amesema.Hata hivyo Kamanda Muroto amesema anasikitishwa na kitendo cha aliyekuwa dereva wa mbunge huyo wakati wa tukio kutoonyesha ushirikiano kwa jeshi la polisi. Tunasikia yupo nje ya nchi na hadi leo hajaitikia wito wa kufika polisi kupata maelezo yake ambayo yangesaidia katika upepelezi wa tukio hilo.”

“Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani yetu”: Waziri Mkuu

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ipo salama na imara na kwamba mtu yeyote atakayejaribu kutaka kuvuruga amani atachukuliwa hatua kali za kisheria. Ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Septemba 13, 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Bw. Mousa Farhang jijini Dar es Salaam. “Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote kutoka popote atakayejaribu kuvuruga amani yetu. Nawaomba wananchi muwe makini na muendelee kuidumisha amani yetu.” Amesema kwa sasa Serikali ipo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi, rushwa, biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na wahujumu uchumi. Waziri Mkuu amesema licha ya Tanzania kuwa ni nchi ya amani na yenye utulivu wa kisiasa, wameendelea kuwahamasisha wananchi wake kudumisha mshikamano. Amesema mbali ya kuimarisha amani nchini, pia Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji jambo ambalo litawawezesha watakaokuja kuwekeza nchini kupata tija. Hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribis