Je unasumbuliwa na tatizo la kutodumu na mpenzi mmoja?fanya haya kuepuka tatizo
Ni matumaini yangu marafiki mtakuwa mko poa na mnaendelea na majukumu ya kazi za kila siku. Kama kawaida kupitia safu hii tunapata kujifunza yahusuyo mapenzi. "Ninapoandika makala haya, najaribu kujenga picha kwa vijana wangu wakali kunako anga la muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba na Judith Wambura ‘Jide’ walipoimba; hakunaga mapenzi yale… kupendana ni zama za kale!... siku hizi kwa kudanganyana, mvulana msichana, ishakuwa poapoa tu ". Kizazi cha zamani hakikupata shida sana katika hili. Kilisubiri muda muafaka ufike ndipo mtu athubutu kufanya maamuzi ya kuingia katika uhusiano ambapo ndani ya muda mfupi basi ndoa ilichukuwa nafasi. Kizazi cha sasa hivi, kimetawaliwa na tamaa, vijana wanaingia katika uhusiano wakipelekwa na tamaa za kimwili pasipo kutazama umri na madhara ya kukurupukia mapenzi. Matokeo yake sasa, ndiyo pale unapoona vijana wanateseka katika kumpata mke au mume wa maisha. Ukweli ni kwamba, tatiz...