Posts

Showing posts from June 24, 2013

MIKOROGO YAMUATHIRI WEMA SEPETU APOTEZA MVUTO....MICHIRIZI YAANZA KUPANDA USONI

Image
Matumizi mabaya ya vipodozi yameanza kumuathiri  wema  Sepetu  ambaye  ni  miss Tanzania  2006.. Wema  ambaye umri wake bado  haujamtupa  , hivi  sasa  anakabiriwa na tatizo la  ngozi  kutokana  na michirizi  kusambaa  mwili mzima  hasa  mapajani....  Kamera  zetu  si  mara  ya  kwanza  kumshuhudia  Mrembo  huyu  akizingirwa  na  uzee  kwani  miezi  kadhaa  nyuma  tuliwahi andika  habari  inayofanana  na  hii  lakini  ikielezea  zaidi  michirizi  ya  mapajani.... Tofauti  na  hivyo, hivi  sasa  michirizi  hiyo   imekimbilia  kifuani  na  mabegani  hali  inayoashiria  kwamba  siku  si  nyingi  itahamia  usoni... "Ukweli  Wema  Sepetu  sasa  amebaki sura  tu,mwili  umemtupa  kabisa .Nadhani  hii  yote  inatokana  na  matumizi  mabaya  ya  mikorogo" ...alisema  shuhuda  mmoja  akimtazama  Wema sepetu  aliyekuwa  jaji  katika  shindano  moja  la  umiss  jijini  Dar Baada  ya  kumsikia  shuhuda  huyo  akimtoa  kasoro  mrembo  huy

MWIGULU NCHEMBA NA MSIGWA NUSURA WATWANGANE NGUMI BUNGENI

Image
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha. Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge wapambanaji na Ukimwi, ambapo baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria, baada ya kutoonekana mjini humo tangu Juni 17 mwaka huu. Wabunge hao wa Chadema hawakuhudhuria kikao chochote cha Bunge kutokana na kwenda mkoani Arusha kwa shughuli mbalimbali, kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wao wa kuhitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika viwanja vya Soweto, Juni 16 jijini humo. Malumbano hayo yanatokana na Nchemba kuituhumu Chadema kuhusika na mlipuko huo, Juni 20 mwaka huu wakati a

HALI YA MANDELA NI TETE...ASHINDWA KUFUMBUA MACHO KWA SIKU KADHAA

Image
Mzee Nelson Mandela ameendelea kuwa katika hali mbaya hospitalini jana baada ya kubainika kwamba gari la wagonjwa lililombeba Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kwenda hospitali limeharibika. Gari hilo la wagonjwa mahututi liliharibika wiki mbili zilizopita wakati Mandela alipokuwa akikimbizwa kwenye hospitali moja mjini Pretoria, na kumwacha 'njiapanda' kwa dakika 40. Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alihamishiwa kwenye gari jingine la wagonjwa la hospitali ya kijeshi kumalizia safari iliyobaki ya dakika 50 kati ya Johannesburg na Hospitali ya Moyo ya Medi-Clinic. Msemaji wa Rais Mac Maharaj alisema: "Tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha kwamba hali ya kiafya ya rais wa zamani Mandela haiathiriki na tukio hilo." Madaktari wanaomtibu Mandela waliridhika kwamba hakupata maumivu yoyote katika kipindi hiki, aliongeza Maharaj. Taarifa ya jana kuhusu afya ya Mandela inaonesha kwamba kuna mabadiliko kidogo katika hali ya shuj

MAAJABU: MTOTO AZALIWA NA MAKALIO MATATU, MAMA YAKE ALIA AKIOMBA MSAADA

Image
Maajabu  ya  uumbaji  yamemfanya  mama  mzazi  wa  Xiao Wei  ambaye  ni  mchina amwage  machozi  akiomba  msaada  wa  kunusuru  maisha  ya  mwanae   mwenye  umri  wa  miezi  7 aliyezaliwa  na  makalio matatu... Kalio  la  tatu  lipo  kama  mkia  mfupi, wenye  urefu  wa   sentimita  8  ( 8 cm ), katikati  ya  makalio  mengine  mawili. Akiongea   kwa  uchungu, mama  mzazi  wa  mtoto  huyo  amedai  kuwa  kwa  muda  mrefu  amekuwa  akiwaomba  madaktari  wafanye  upasuaji  wa  tako  hilo  lakini  wao  wamekuwa  wakimjibu   kuwa  hiyo  si  kazi  nyepesi  kama  anavyodhani.... "Tukilikata  litaota  tena, hivyo  hatutakiwi  kukurupuka  na  badala  yake  tutakiwa  kupata  muda  wa  kupitia  vitu  vingi  ukiwemo  mrija  wa  uti  wa  mgongo  ambapo  kalio  hilo  limejiegesha" ...Alisema  daktari  mmoja  akimjibu  mama  huyo

"TUNAJIANDAA KUIPINDUA NCHI ENDAPO SERIKALI HAITAWASHUGHULIKIA WATU WALIOFICHA MABILIONI USWISWI"...ZITTO KABWE

Image
Zitto  Kabwe  amefunguka  na  kudai  kuwa  kwa  sasa  wanajiandaa  kufanya  mapinduzi  ya  nchi   endapo   watu  walioficha    mabilioni  uswiswi    hawatashughulikiwa  ipasavyo.... Suala la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.    Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.   Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge. Zitto  Kabwe  anatoa  angalizo  katika  hatua  hiyo  ya jaji Werema   kwa  kusema  kuwa  hatua  hii  isiwe  "zima  moto"   na  daganya  toto  ili  kuwafumba  macho

NGONO KINYUME NA MAUMBILE ZAONGEZEKA TANZANIA ....WENGI WAO WANAFANYA KUONDOA MIKOSI

Image
Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Nchini (Tacaids) imesema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa vitendo vya ngono kinyume na maumbile vinazidi kuongezeka. Hayo yalisemwa jana na Dk. William Kafura, katika mkutano wa sita wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Ukimwi (Tapac). Alisema hiyo inatokana na imani za kishirikina kwamba wakifanya vitendo hivyo watapata bahati kwa kupandishwa vyeo. “Lazima tukubali tatizo lipo na tulitafutie suluhisho, utafiti upo umefanywa na Muhimbili, umefanywa na chuo kikuu cha Dar es Salaam, umefanywa na Tasisi ya Utafiti ya Ifakara,” alisema. Alisema pia wafanyabiashara wanaamini kwa kufanya vitendo hivyo watajirika wakati wanawake wanaamini kuwa watazidi kupendwa. Kwa upande wake Mwenyekiti wa TACAIDS, Dk. Fatuma Mrisho, alisema utafiti uliofanyika nchini unabainisha kuwa wanawake hawana uelewa wa kutosha juu ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi. Akizungumzia suala la kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi Dk. Mrisho alisema kuwa wanaume wana uelewa