Posts

Showing posts from June 20, 2015

Lowassa Apata Mapokezi ya Kishindo Jijini Mbeya..Apata Wadhamini 53,156 Toka Mkoani Mbeya

Image
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache na kutoa shukrani kwa WanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya, leo Juni 19, 2015. Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, wakiwa wamemzunguka Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati) wakati alipowasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya leo Juni 19, 2015 kukabidhiwa fomu zitakazomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mbeya wamevunja rekodi ya udhamini kwa Mh. Lowassa ya mikoa yote aliyopita, amepata wadhamini 53,156 kwa mkoa wa Mbeya pekee.   Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM zaidi ya elfu tisa wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kutoka kwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Mar...

Neymar afungiwa mechi nne na bonge la faini

Image
Nyota wa Brazil na klabu ya Barcelona Neymar hatocheza tena michuano ya Copa America inayoendelea huko Chile baada ya kufungiwa kucheza mechi nne kutokana na kitendo chake cha utovu wa nidhamu alichokifanya wakati Brazi ikicheza dhidi ya Colombia mchezo ambao ulimalizika kwa Brazil kufungwa kwa goli 1-0. Nahodha huyo wa Brazil alioneshwa kadi nyekundu baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi kupulizwa kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Santiago Jumatano iliyopita. Neymar alimpiga na mpira mgongoni kwa makusudi mchezaji Pablo Armero wa Colombia mara baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya mwisho kumaliza mchezo huo. Mshikemshike baada ya Neymar kuzua tafran kwa kupiga mpira ulio ‘mbabua’ mgongoni mchezaji wa Colombia Awali alifungiwa kucheza mechi moja, lakini baadae shirikisho la soka la Amerika ya Kusini (South America Football Confederation) liliongeza kifungo na faini ya dola 10,000 za Kimarekani baada ya Neymar kugundulika kuwa alimtolea maneno machafu m...

CHILE YAIUA BOLIVIA 5-0, SANCHEZ KAMA KAWAIDA

Image
Chile imetoa kipondo cha mbwa mwizi kwa Bolivia baada ya kuichakaza kwa jumla ya bao 5-0 ikiwa ni mchezo wa kundi A kwenye michuano ya kombe la Mataifa ya bara la America Kusini almaarufu kama Copa America mchezo uliomalizika alfajiri ya leo huko nchini Chile. Charles Aranguiz alianza kuipatia Chile bao la mapema ikiwa ni dakika ya tatu tangu mchezo huo kuanza kabla ya winga wa Arsenal Alexis Sanchez kufunga goli la pili dakika ya 37 na kuifanya Chile iende mapumziko ikiwa mbele kwa goli 2-0 dhidi ya Bolivia. Kipindi cha pili kilikuwa kibaya zaidi kwa Bolivia kutokana na Chile kulisakama lango lao kwa muda mwingi wa mchezo hali iliyopelekea wafanye makosa mengi kwenye safu yao ya ulinzi na kutoa mianya kwa Chile kufunga mabao. Aranguiz alipachika pao la tatu kwa Chile dakika ya 66 lakini likiwa ni bao lake la pili kwenye mchezo huo, kabla Gary Medel hajatupia nyavuni goli la nne dakika ya 80. Zikiwa zimebaki dakika nne ili mwamuzi amalize pambano hilo, Ra...

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AUNGURUMA WILAYANI BUSANDA NA MJI MDOGO WA KATORO MKOANI GEITA LEO.

Image
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Katoro, wakati wa ziara Jimbo la Busanda, wilayani Geita, Mkoa wa Geita, ambapo aliwaahidi wachimbaji wadogo wadogo kulitafutia ufumbuzi wa kuwapatia vitalu vya machimbo eneo la Nyarugusu linalomilikiwa na Stamico, wilayani Geita. Ndugu Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, yupo mkoani Geita kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. eneo la Nyarugusu. 

ALIYETEKA ALBINO TABORA AFUNGWA JELA MIAKA 10

Image
Masanja Mwinamila (44) mara baada ya kufikishwa katika kituo cha Polisi Wilaya ya Nzega Juni 15, 2015. Mtoto Margreth Hamisi Machiya (6) aliyenusurika kuuzwa akiwa hai na mjomba wake. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Juma Bwire akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo Juni 16, 2015. Na Daniel Mbega, Nzega. MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Nzega leo hii imemhukumu Masanja Mwinamila (44), mkazi wa Kitongoji cha Kona Nne, Kijiji cha Ugembe II, Kata ya Mwakashanhala, Tarafa ya Puge wilayani Nzega katika Mkoa wa Tabora kwenda jela miaka 10 kwa kosa la kuteka mtoto mwenye albinism, Margreth Hamisi (6). Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Saraphine Nsana, alitoa hukumu hiyo baada ya mshtakiwa kusomewa shtaka na kukiri kutenda kosa hilo. Ilielezwa mahakamani hapo kwamba, mnamo Juni 15, 2015 majira ya saa 3:00 usiku katika Kijiji cha Ugembe II, Kata ya Mwakashanhala wilayani Nzega, mtuhumiwa alimteka binti huyo kw...

RAIS KIKWETE KATIKA ZIARA YA KISERIKALI NCHINI INDIA

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakiweka shada katika kaburi la mpigania uhuru na muasisi wa taifa la India Mahatma Ghandi jijini New Delhi India leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi mara baada ya kuwasili Ikulu ya India kwa sherehe za ukaribisho wake rasmi nchini India kwa ajili ya ziara yake ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika asubuhi ya leo, Ijumaa, Juni 19, 2015. Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu wa IndiaMheshimiwa Narendra Modi, na Rais Wa IndiaMheshimiwa Pranad Mukherjee wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya Rais kikwete kuwasili katika ikulu ya India kwa mapokezi rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono  na Rais wa India, Mheshimiwa Pranad Mukherjee (kushoto) na Waziri Mkuu, Mheshimiw...