Posts

Showing posts from February 5, 2016

BREAKING NEWS : FREEMAN MBOWE ATANGAZA BARAZA KIVULI LA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI,

Image
Freeman Mbowe na mawaziri Vivuli.  Ofis ya rais Tamisemi jafar maiko Utumishi Lucy molel Makam muungano Ali saleh A. Ali PM bunge kazi na ajira Esta bulaya Sera na mipango Halima mdee Naibu silinde Uchukuzi Injinia mbatia Will kambalo Nishat  Mnyika na heche Maambo ya nje Msigwa Kilimo Makdalena sakaya Ulinzi Juma hamad omar Waitara naibu Mambo ya ndani Lema Ardhi Wilfred lwakatare Maliasili Estamatiko na pareso Viwanda Kalist komu Elimu Suzan limo Afya Dk godwin molel Habar  Joseph mbiliny Minja devota Maji Hasan bobali Peter lijualikali Katiba na sheria Tundu lisu

Aliyedaiwa kumbaka shilole afunguka mazito!

Image
  Makala Elia Joseph. Makala: richard manyota -igunga KATIKA maho-jiano na Mwandishi nguli wa burudani nchini wa Gazeti la Ijumaa, Erick Evarist, Februari 2012, msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ alinukuliwa akieleza kisa hiki: “Katika maisha yangu nimepitia mitihani mingi, mmoja wapo ni huu wa kulazimishwa kufanya mapenzi bila ridhaa yangu, kwa kifupi nilibakwa.” Kwa kuwa kisa hiki cha kusikitisha kimesemwa sana na Shilole katika mahojiano yake mengi na vyombo mbalimbali vya habari, Gazeti la Ijumaa lililazimika kufunga safari mpaka wilayani Igunga mkoani Tabora ili kumtafuta anayetuhumiwa kumbaka ambapo lilifanikiwa kufanya naye mahojiano. UTAMBULISHO WA JINA NA MAKAZI “Kwa jina naitwa Makala Elia Joseph. Nimezaliwa mwaka 1988 ni mtoto wa pili katika familia yetu. Naishi hapa Igunga, karibu na stendi ya mabasi yaendayo mikoani eneo la Barabara ya Singida. Mwandishi: Umejitambulisha vyema. Mimi ni Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Ijumaa, nimetoka Dar…(Kicheko kinakati

Mbunge adatishwa na penzi la Lungi

Image
Msanii maarufu wa filamu Bongo, Lungi Maulanga. Hamida Hassan na Gladness Mallya Taarifa ambayo gazeti hili linayo ni kuhusu mbunge moja machachari sana wa chama tawala (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye kwa muda mrefu amekuwa akidaiwa kutoka kimapenzi kwa siri na msanii maarufu wa filamu Bongo, Lungi Maulanga. Chanzo makini ambacho kipo karibu na Lungi kimeeleza kuwa, Lungi na mheshimiwa huyo wamekuwa ‘lovers’ kiasi cha kufikia kila mmoja kufa na kuoza kwa mwenzake. Kisikie chanzo “Yaani suala la mheshimiwa (anataja jina la mbunge huyo) kutoka na Lungi siyo siri na wakati mwingine Lungi mwenyewe anajitapa kuwa sasa hivi ni matawi ya juu, nyie fuatilieni mtajua ukweli.” Ijumaa laingia mzigoni Kufuatia madai hayo, Ijumaa liliingia mzigoni kujaribu kuwafuatilia wawili hao hasa inapobainika mheshimiwa huyo yuko jijini Dar lakini hawakuweza kunaswa, hali iliyoonesha kuwa, huwa wanakutana kwa siri sana. Hata hivyo, rafiki huyo wa Lungi juzikati alimpigia simu mmoja wa

EDWARD LOWASSA AUNGA MKONO MAAMUZI YA CUF KUTOSHIRIKI UCHAGUZI ZANZIBAR

Image
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananch UKAWA, Mh. Edwrad Lowassa amesema ni vema serikali ikahakikisha inapata suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio machi 20 mwaka huu. Mh. Edward Lowassa amesema hayo ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na wazee kutoka chama cha Chadema ambapo amesema  anaunga mkono uongozi wa CUF kutokushiriki uchaguzi huo huku akisisitiza endapo serikali ikishindwa kumaliza mgogoro huo kabla ya mach 20 huenda hali ya kisiasa Zanzibar ikabadilika. Aidha amewahakikishia wazee hao kuwa yeye na uongozi mzima wa UKAWA wako imara katika kuhakikisha wanatetea maslahi ya watanaznia ambapo pia amemshukuru waziri mkuu kwa kuruhusu mikutano suala ambalo linawapa fursa ya kujipanga ili kuwashukuru watanzania waliojitokeza kupiga kura mapema 25. Kwa mujibu wa risala ya wazee hao iliyosomwa na mzee Enec Ngomba

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI MGENI RASMI SIKU YA SHERIA NCHINI, ASISITIZA UFANISI WA MAHAKAMA NA UTOAJI WA HAKI KWA WAKATI

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini. Rais, Dkt. John Magufuli alikua mgeni rasmi.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria leo jijini Dar es salaam.  Wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  (Kulia) akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  Baadhi ya Viongozi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa. Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga, Jaji Kiongozi wa Tanzania Mhe. Shaaban Lila (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Sa

MAGAZETI YA LEO IJUMAA

Image