Ujenzi wa kituo cha Afya Dongobesh awamu ya pili waendelea kutekelezwa kwa zaidi ya aslimia 80- Mbulu
muonekano wa jengo la wodi ya mama na mtoto kituo cha Afya Dongobesh likiwa katika hatua ya ukamilishaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu inategemea kukamilisha ujenzi wa majengo matano ya kituo cha Afya Dongobesh ifikapo Juni 30 2018, hatua hii imefikiwa ikiwa ni utekelezaji wa kiwango cha aslimia 80 kilichobainishwa baada ya kufanyika ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Dongobesh,tathimini hiyo ilitolewa na timu ya Wataalam toka Tamisemi, wakilishirikiana na wataalam toka Mkoa wa Manyara . Timu ya wataalam wakiwa katika moja ya majengo mapya ya kituo cha afya wakiendelea na ukaguzi. Timu hizo ziliweza kufanya ukuaguzi wa majengo hayo mapya yanayoendelea kukamilishwa kabla ya Mwezi Juni kukamilika ili kubaini kama kiasi cha fedha Tsh. Milioni 400 zilizotolewa na Serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo unakamilika kwa wakati. Mgawao huo wa fedha uliotolewa ikiwa na mgawao aw...