Watu 3200 wakusanyika na kupigwa picha za utupu!
Sehemu ya umati wa watu 3,200 waliohudhuria tukio hilo. Hull, Uingereza WATU zaidi ya 3200 wamekusanyika na kusherehekea utamaduni wao wakiwa kwenye huku wakiwa wamevua nguo zao zote (utupu) katika Mji wa Hull, Uingereza ikiwa ni tukio la kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni. Katika tukio hilo lilitokea Jumamosi ambapo washiriki walijipaka miili yao rangi ya bluu-baharina kisha kupigwa picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull. Mradi huo unatekelezwa na mpiga picha Spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya Sanaa ya Ferens Art Gallery. Picha zilizopigwa siku ya tukio hilo, zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka mmoja. Tunick, anayetoka New York, amewahi kupiga picha za watu wengi wakiwa uchi Sydney Opera House, Place des Arts mjini Montreal, Mexico City na mjini Munich nchini Ujerumani Ger...