Posts

Showing posts from April 10, 2016

Msanii Mwigine wa Bongo Anayeteketea Kwa Madawa ya Kulevya Huyu Hapa....

Image
Wauza unga kuweni na huruma kwa watanzania wenzetu,yule Dogo Mfaume wa enzi zile za "kazi yangu ya dukani" ndo basi tena sasa hivi kashakua teja....daah vipaji vya ukweli vinazidi kupotea kwa ngada. Mlaaniwe wote mnaouza unga kuanzia nyie wenyewe na vizazi vyenu vyote. ..."kazi yangu ya dukanii aaahahh yaniweka matataniii wanao nirudisha nyuma wengi wao majiraniii"

Msafara wa Rais Magufuli Kutozidi watu 10.....Balozi Mahega Asema Anategemea Kwenga Ng'ambo hivi Karibuni

Image
Rais John Magufuli anataraji kusafiri tena kwenda nje ya nchi hivi karibuni akiwa na msafara ambao unawezekana usizidi jumla ya watu 10. Ilimchukua Rais Magufuli siku 153 tangu kuapishwa kwake kufanya ziara ya kwanza ya nje ya nchi baada ya kwenda Rwanda kwa mwaliko wa Rais Paul Kagame Jumanne iliyopita. Rais alikwenda Rwanda kwa ajili ya kufungua daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha biashara chenye huduma za pamoja, ambacho ni kiunganishi muhimu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika safari hiyo, katika kile kinachoonekana kuwa ni muendelezo wa hatua yake ya kubana matumizi ya serikali kadri iwezekanavyo, Rais Magufuli alikuwa na msafara usiozidi watu 10. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Mahiga, alisema jana kuwa Rais Magufuli anatarajia kusaifiri tena kwenda nje ya nchi hivi karibuni. Balozi Mahiga alisema katika safari hiyo, msafara wake utaendelea kuhusisha watu wachache w

Mrema wa TLP Amuomba Rais Magufuli Atimize Ahadi yake ya Kumpa KAZI Kama Alivyokuwa Amemwahidi Wakati wa Kampeni

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema amemuunga mkono Rais John Mgufuli kwa kasi yake ya kupambana na ufisadi na kumuomba ampe kazi ili amsaidie kutekeleza jukumu hilo. Mrema alimuomba Rais Magufuli atambue uzoefu wake kwa kukumbuka jinsi alivyopambana na mafisadi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu. Huku akieleza CV yake hiyo, Mrema alimkumbusha Rais kuhusu ahadi aliyompa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, ya kumpa kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa atashinda na kuwa Rais. Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro, Mrema alisema kuwa anasikitishwa na ukimya wa Rais Magufuli kwa sababu aliamini kuwa angetekeleza ahadi hiyo ya kumpa kazi muda mfupi baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri, jambo ambalo hadi sasa hajalifanya. Alisema, alikutana na Rais Magufuli mwaka jana katika kampeni jimboni Vunjo kwenye eneo la Njia Panda l

Huyu Ndiye Rubani wa Kwanza Mwanamke Tanzania Kurusha Boeing Airbus

Image
KATI ya wanawake wa Kitanzania waliopeperusha bendera yetu vizuri nje ya nchi kielimu ni Kapteni Hilda Wendy Ringo ambaye sasa ni rubani. Elimu yake ya sekondari aliipata katika Shule ya Tambaza jijini Dar es Salaam na baadaye Chuo Cha Urubani cha Progress Flight Academy cha jijini Pretoria, Afrika Kusini. Ni mwanamke wa kujivunia katika nchi yetu kwa sababu amekuwa akirusha ndege yaani rubani. Amewahi kuhojiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini na kuhusu kazi yake hiyo anasema: “Kurusha ndege ni jambo zuri linalofurahisha.” Rubani Hilda ni mama mwenye umri wa miaka 33, anasema alianza kurusha ndege akiwa na umri wa miaka 22 lakini sasa anarusha ndege hapahapa nchini katika Kampuni ya Precision Air. Ana uzoefu mkubwa na kazi hiyo ya urubani kwa sababu ameifanya kwa zaidi ya miaka 10 sasa na ni mwanamke wa kwanza Mtanzania kurusha ndege aina ya Boeing Airbus. Anasema wazo la kuwa rubani lilimuingia katika akili yake akiwa bado mdogo baada ya kujiuliza m

Waziri Mkuu Majaliwa ashiriki mazishi ya kaka yake

Image
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo kwenye kaburi la kaka  yake, Selemani Selemani katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji cha  Narung’ombe wilayani Ruangwa Aprili 9, 2016.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBLEA HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua mashine ya MRI katika hospitali ya Benjamin Mkapa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma wakati alipoitembela Aprili 9, 2016. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, , Dkt. Hamis Kigwangala. Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Khamis Kigwangala wakikagua mashine ya Mobile Digital xray wakati walipotembelea hospitali ya Benjamin Mkapa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma Aprili 9, 2016.Kulia ni Kaimu Mkuu wa Hospitali hiyo ProfesaGesai. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)