Posts

Showing posts from February 20, 2018

Breaking: Ripoti ya TRA Kuhusu Utajiri wa Kakobe, Amuomba Radhi JPM

Image
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema wakati wakiendelea kumchunguza Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel, Zachary Kakobe , mnamo Januari 24, 2018, Askofu huyo alimuandikia barua Rais Dkt. John Magufuli kumuomba radhi kutokana na kauli yake ya kebehi na matamshi ya dharau kuwa ‘ana pesa nyingi kuliko Serikali’. Hayo yamesemwa leo na Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere , wakati akizunumza na wanahabari jijini dar es Salaam akitoa ripoti ya uchunguzi huo. Akihubiri wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi, Desemba 24, mwaka jana, askofu huyo alisema yeye ni tajiri zaidi ya serikali ya Tanzania na baadaye kusema kuwa utajiri anaomiliki kwa sasa ni zaidi ya serikali nyingi duniani jambo ambalo liliwafanya TRA wamchunguze.

RATIBA KUAGWA MWILI WAMAREHEMU AKWILINA DAR

Image
BAADA ya maridhiano ya kuuchukua mwili katika Hospitali ya Taifa Mhimbili, familia ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi imetoa ratiba ya kuagwa kwa mwili w binti huyo. Akizungumza baada ya kupokea ripoti ya mwili wa marehemu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kaka wa marehemu, Moi Kiyeyeu alisema kuwa mdogo wake ataagwa Alhamisi hii Februari 22, katika viwanja vya Chuo cha NIT kilichopo Mabibo jijini Dar na baadaye atasafirishwa kwenda nyumbani kwao Rombo-Mashati mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi. Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, ripoti ya uchunguzi waliyopewa na madaktari wa Muhimbili inaonesha kuwa marehemu alipigwa risasi kichwani iliyoingia upande wa kushoto na kutokea upande wa kulia. “Ripoti tuliyopewa inaonesha kichwa cha marehemu kilipasuliwa na risasi ambayo iliingia upande wa kushoto na kutokea upande wa kulia ambao umefumuliwa vibaya,” shemeji wa Akwilina, Festo Kavis

Mbowe, Mashinji, Mnyika na Wengine 4 Waitwa kwa DCI Kuhojiwa

Image
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na viongozi wengine 6 wa chama hicho wameitwa rasmi Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa. Viongozi hao wanatuhumiwa kwa kufanya maandamano kinyume cha sheria kwa mujibu wa barua hiyo ya wito kutoka kwa Jeshi la Polisi. Viongozi wengine 6 walioitwa ni; – Dkt Mashinji(Katibu Mkuu wa CHADEMA) John J. Mnyika(Mbunge na Naibu Katibu Mkuu Bara) Salum Mwalim(Naibu Katibu Mkuu ZNZ) Halima Mdee(Mbunge na M/Kiti wa BAWACHA) John Heche(Mbunge) Ester N. Matiko(Mhazini wa BAWACHA).

ZARI KUMPIGA KIBUTI DIAMOND KWAIBUA MAMBO MAPYA,KWANINI ZARI KAUMIZWA UJEREO WA WEMA SEPETU NA SI HAMISA MOBETO

Image
SIKU chache baada ya Zarinah Hassan ‘Zari Boss Lady’ kuweka wazi kuwa ameachana na baba watoto wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, swali linakuja ni kwa nini Zari anaweza kuwa ameumizwa sana na Wema Abraham Sepetu na si Hamisa Mobeto ambaye hivi karibuni amempa msongo wa mawazo baada ya kuzaa na baba watoto wake? Twende taratibu! Kwanza nauliza swali hilo ambalo nitaliweka wazi baadaye kidogo na kadiri unavyoendelea kusoma makala haya, utanielewa. Baada ya matukio yote ya Diamond na Mobeto, bado Zari alionekana kuwa ‘jiwe’ na kutetea penzi lake lakini lilipokuja suala la shoo ya Mboso ambayo Diamond alionekana wazi kuwa na mahaba na Wema kwa video yao ya ‘kupapasana’ kuwekwa mitandaoni, siku chache baadaye Zari aliamua kutangaza rasmi kummwaga Diamond. Sababu ya wadau na mashabiki wa Baba Tiffah na Mama Tiffah kuona kuwa hiyo itakuwa imemuudhi Zari ni jinsi wapendanao hao walivyopotezeana hata kabla ya Zari kutangaza kuachia ngazi na muda mwingi akaonekana kuu

Mke na Mme Waliokamatwa na Madawa China, Familia Yaanika A-Z

Image
Baraka Malali na mkewe pamoja na mtoto wao. Sakata la Watanzania wawili ambao ni mke na mume kukamatwa na dawa za kulevya ‘unga’ nchini China na mtoto wao kurudishwa Bongo , limeingia sura mpya, baada ya familia za pande zote mbili kuzungumza na siri ya safari yao kufichuka, Ijumaa Wikienda lina ukweli wa tukio hilo. Wakazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam , Baraka Malali na mkewe Ashura Musa walikamatwa Januari 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Baiyun jijini Guangzhou, China wakiwa wamemeza jumla ya pipi 129 za dawa za kulevya zilizosadikika kuwa ni heroin. Mume alipakia pipi 47 na mkewe pipi 82. Taarifa zilieleza kuwa, mamlaka nchini humo ziliamua kumrudisha nyumbani mtoto wao ambaye aliwasili Bongo wikiendi iliyopita kukabidhiwa kwa Ustawi wa Jamii, wakati mipango ya kumkabidhi mtoto huyo kwa ndugu wa wazazi wake ikiendelea. Baada ya kujiri kwa tukio hilo, Ijumaa Wikienda lilizungumza na wazazi wa watuhumiwa hao na Idara ya Ustawi wa Jamii kujua kw