Posts

Showing posts from March 8, 2018

Wakali Wanne wa Kimataifa Waitwa Taifa Stars

Image
KOCHA wa Timu ya Taifa ya Soka Tanzania (Taifa Stars), Salum Mayanga, leo Machi 8, ametaja majina ya wachezaji 23 watakaoingia kambini kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki mwezi huu. Katika orodha hiyo aliyoitaja asubuhi hii kwenye makao makuu ya shirikisho la soka nchini TFF Karume Ilala, Mayanga amewajumuisha kikosini nyota wanne wa kimataifa akiwemo nahodha Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu anayechezea klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden, Mlinzi wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda na Faridi Mussa anayechezea Club Deportivo Tenerife ya Hispania. Katika majina hayo 23, Simba imechangia wachezaji 6, Yanga ikitoa wachezaji 5 huku nahodha wa Singida United, Mudathir Yahya naye akijumuishwa kikosini. Taifa Stars inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki ikianzia ugenini nchini Algeria, Machi 22 dhidi ya wenyeji, The Greens kabla ya kurejea nyumbani, Dar es Salaam kuwakaribisha DR Congo, Machi 27, katika Uwanja wa Taifa.

Naibu Wazri Ikupa atekeleza ahadi yake

Image
Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu, Mh. Stella Ikupa leo amefanya ziara ya ya kutembelea shule ya Sekondari Jangwani, Uhuru Mchanganyiko na Pugu jiji Dar es salaam na kukabidhi  vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu  . Katika ziara hiyo Mh, Ikupa ametoa Magongo ya kutembelea, viti mwendo, fimbo nyeupe kwa wasiona, miwani ya jua, kofia, lenzi za kusomea kwa watu wenye uono hafifu, na ualubino ili kutatua changamoto kwa kundi hilo maalumu. Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu Mh Stella Ikupa akimkabidhi baiskeli mwendo mwanafunzi wa Pugu Sekondari Naibu Waziri  Ikupa amesema kama Serikali tunatambua changamoto hizi hivyo tunajitahidi kukabiliana nazo na kidogo kinachopatikana tunakigawa kwa kila mmoja ili kupunguza matatizo haya kidogokidogo na mwisho wa siku yataisha. Pia serikali hii inayoongozwa na Rais Magufuli itaendelea kutennga fedha kwa ajili ya kuendeleza kuwahudum...

Manyara: Mbunge CCM Ahojiwa Sentro kwa Amri ya DC

Image
MBUNGE wa Jimbo la Hangang kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mary Nagu amehojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Sara Ali,  kwa kile kinachodaiwa kukaidi amri halali ya DC ya kuzuia mikutano ya mbunge huyo. Inadaiwa Nagu na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Mathew Darema, waliwekwa ndani kwa saa kadhaa juzi kabla ya kuhojiwa. Ikumbukwe kuwa, hii ni mara ya pili sasa kwa tukio kama hili kujitokeza kwa  Nagu wilayani humo ambapo Mara ya kwanza DC Sara aliwafikisha polisi Katibu wa CCM Wilaya na Mbunge wake kwa madai kuwa walifanya fujo katiika Kikao cha Kamati ya Siasa cha Wilaya. CREDIT: JF

AJIRA SERIKALINI: MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)- INTERNAL AUDITOR II

Image
INTERNAL AUDITOR II – 2 POST Employer:  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Date Published:  2018-03-05 Application Deadline:  2018-03-19 JOB SUMMARY: N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES: i. Participates in audit assignments of the Fund, including pre auditing of providers’ claims and Board claims/payments; ii. Assists to inspect validity of vouchers, receipts, payments, cheque registers and their respective source documents; iii. Assists to check bank reconciliation statements; iv. Assists in auditing journals and other accounting entries; v. Participates in inspection of goods/stocks received and verifies stock records in the store; vi. Assists in performing all his day to day duties as stipulated and specified in the job description of that position; vii. Assists to review imprests retired, checking adherence to imprests regulations, validity of receipts (if any) and performing any other related clerical works; and viii. Performs any other re...

AJIRA SERIKALINI: Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)- ACCOUNTANT II

Image
ACCOUNTANT II – 1 POST Employer:  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Date Published:  2018-03-05 Application Deadline:  2018-03-19 JOB SUMMARY: N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES: Accountant II– Expenditure i. Ensures that all payments are made in accordance with financial regulations and approved budget; ii. Maintains Zonal administrative imprest accounts and ensures timely refunds and replenishments; iii. Oversees the management of the petty cash account; iv. Oversees maintenance of the non-current assets register; v.  Prepares financial statements; vi. Prepares periodic reports on the status of expenditure; vii. Administers and maintains non-current assets register; viii. Maintains subsidiary legers for staff loans; ix. Monitors imprest returns from Zonal offices and takes corrective actions whenever necessary; x. Maintains ledgers for imprest; xi. Monitor and control of salary advances; xii. Deals with all issues pertaining to rep...

Breaking News:Abdul Nondo apatikana Mafinga mkoani Iringa

Image
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliyekuwa hajulikani alipo tangu usiku wa kuamkia jana na kuacha ujumbe usemao “I AM AT HIGH RISK”, amepatikana Mafinga mkoani Iringa. Mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Paul Kisabo amesema  kwamba Abdul Nondo amepatikana mkoani Iringa katika wilaya ya Mafinga jana jioni baada ya kuzinduka na kujikuta ametupwa barabarani. “Nondo amepatikana Mafinga katika Kituo cha Polisi hivi punde, amezinduka na kujikuta akiwa ametupwa, akauliza watu eneo alipo ndipo wakamwambia yupo Mafinga, amejikokota na kuelekea kituo cha polisi kuripoti. “Kilichomsaidia alikuwa anakumbuka namba mojaya dada yake ambayo alikuwa ameikariri kichwani, ikabidi aombe simu polisi, kumpigia dada yake ambaye naye alijulisha baba yake mdogo aliyepo Dar es Salaam kuwa ndugu yao amepatikana. “Nondo ameongea na baba yake mdogo kupitia simu ya p...